4x4

Clinton akataa kushiriki mdahalo Marekani


SandersImage copyrightGETTY
Image captionSanders amesema hajashangazwa na uamuzi wa Clinton
Mgombea urais anayeongoza katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton amekataa kushiriki mdahalo wan ne dhidi ya mpinzani wake Bernie Sanders.
Maafisa wake wa kampeni wamesema badala yake, Bi Clinton ameonelea ni heri kukabiliana na mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump.
Bi Clinton alikuwa awali amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.
Bw Sanders, Seneta wa Vermont, amesema hajashangazwa na uamuzi huo wa mpinzani wake.
Na katika hatua inayoonesha viongozi wa Democratic hawataki kumtenga Bw Sanders na wafuasi wake, wametangaza kwamba mgombea huyo ataruhusiwa kuteua theluthi moja ya kamati ya kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwezi Julai.
Mkutano huo hutumiwa kuidhinisha mgombea urais wa chama cha Democratic.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.
Post a Comment