DKT. MENGI ATOA DARASA KWA WASHIRIKI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA


Mwenyekiti Mtendaji wa Makapuni ya IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama (hawapo pichani) katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) kutoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama chuoni hapo.
 
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi akitoa muhadhara kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuhakikisha usalama wa taifa kwa washiriki wa kozi ya mbinu za kiusalama katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa kilichopo Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
.(Picha zote na Modewjiblog). 
 

IMELEZWA jukumu la ulinzi na usalama kwa dunia ya sasa halimo kwenye mikono ya polisi na wanajeshi pekee bali ni la kila mtu katika nafasi aliyopo kama amani na demokrasia inatakiwa kuendelea kuwapo.Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa, Meja Jenerali Yacoub Mohamed wakati akizungumza na Modewjiblog ofisini kwake baada ya mhadhahara ulioshirikisha wataalamu wa masuala ya habari kutoka sekta binafsi na umma ambao wanachukua kozi ya mbinu za usalama chuoni hapo.

“Zamani mambo ya usalama yalikuwa ya wanajeshi na Polisi lakini kwasasa mambo ni tofauti, kila mmoja anatakiwa kuhakikisha anakuwa mlinzi ili uwepo usalama wa kutosha kwahiyo tunaamini washiriki wakirudi vituoni kwao watazingatia usalama.

“Wote wanaokuja hapa wanakuwa ni viongozi au viongozi watarajiwa na kama sasa tuna wanafunzi 38, 12 sio Watanzania ni kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Malawi, Namibia, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Nigeria na China,” aliongeza Meja Jenerali Mohamed.

Wataalamu walioendesha mihadhara hiyo ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Ltd, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi ambaye amepata nafasi ya kutoa elimu kuhusu habari kwa sekta binafsi na Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC) na mwanazuoni Dk. Ayoub Rioba ambaye aliwasilisha sekta ya umma.

Akielezea ujio wa Dk. Mengi chuoni hapo, alisema wamekuwa na taratibu wa kukaribisha watu mbalimbali ambao wanawaona wana uwezo wa kuelezea uzoefu wao katika mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwa na faida kwa washirika.Alisema chuo chao kimekuwa hakina walimu wa kudumu hivyo pamoja na kutumia watu mbalimbali kama walivyofanya kwa Dk. Mengi pia wamekuwa wakiwatumia walimu wa vyuo vikuu ili kutoa elimu ambayo itawasaidia washiriki katika masomo yao ambayo wanayapata chuoni hapo.

“Chuo chetu hakina walimu wa moja kwa moja kwahiyo huwa tunatumia walimu kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini lakini pia huwa tunakaribisha watu maarufu wanakuja ku’share’ uwezo wao kwa washiriki ambao wanakuwa wapo masomoni.“Dk. Mengi ameshafika hapa chuoni mara tatu na sio mtu wa kwanza kuja alishakuja Pius Msekwa, Mawaziri, Katibu Mkuu kiongozi na hata jana tulikuwa na (Dkt. Ayoub) Rioba,” alisema Meja Jenerali Mohamed.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.