FIFA IMETANGAZA KATIBU MKUU WA KWANZA MWANAMKE MWAFRIKA


Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA May 13 2016 limetangaza kwa mara ya kwanza katibu mkuu mwanamke katika historia ya shirikisho hilo, FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura kutokaSenegal kuwa katibu mkuu wa kwanza wa shirikisho la hilo mwanamke.
Fatma Samba Diouf Samoura anaingia FIFA mwezi June kuanza kazi rasmi na kurithi nafasi ya Jerome Valcke katibu mkuu wa shirikisho hilo aliyefungiwa miaka 12 kutokujihusisha na soka, Samoura mwenye miaka 54 ametangazwa leo katika mkutano uliofanyika Mexico.
Rais wa sasa wa FIFA Gianni Infantino
FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura ambaye CV yake inaonesha kuwa amewahi kufanya kazi katika umoja wa mataifa UN kwa miaka 21, mabadiliko hayo yamefanyika ikiwa ni muendelezo wa mabadiliko katika shirikisho hilo, baada ya Rais wa zamani wa shirikisho hilo Sepp Blatter kuachia ngazi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*