HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.tv: Waziri mkuu Kasim Majaliwa amesema mkutano wa kimataifa uliojadili tatizo la rushwa duniani ni kiashiria kwamba rushwa ni janga la kimataifa na linataka juhudi za pamoja kupambana nalo. https://youtu.be/NmoPPurrmNA

SIMU.tv: Baraza la madiwani katika halmashauri ya Gairo wamesusia kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya halmashauri hiyo kwa madai ya kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri ya Gairo. https://youtu.be/fcR1xNbBfdA  

SIMU.tv: Mkurugenzi wa mfuko wa uwezeshaji wa taifa Edwin Chrisant amewatahadharisha wajasiriamali wote watakaopatiwa fedha za mkopo zitakazotolewa na rais Dr John Pombe Magufuli kuzifanyia kazi iliokusudiwa ili kuinua pato lao. https://youtu.be/5DG_wz9W5uo  

SIMU.tv: Serikali imelipongeza baraza kuu la waislamu kupitia taasisi zake za elimu kwa kutoa mchango mkubwa wa walimu ambao wanasadia katika sekta ya elimu nchini. https://youtu.be/qHr5sABdLtE

SIMU.tv: Hatimaye mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga wamekabidhiwa kombe lao baada ya mchezo wake dhidi ya Ndanda Fc ya Mtwara ambapo walitoshana nguvu kwa kufungana mabao mawili kwa mawili.https://youtu.be/H4TKNRrET5Q

SIMU.tv: Baadhi ya wanafunzi wilayani sengerema mkoani Mwanza wanalazimika kukaa chini kwa kukosa madawati katika baadhi ya shule wilayani humo; https://youtu.be/ZzhMb8kI_rU

SIMU.tv: Wafanyabiashara wa mbao manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wajitolea mbao 350 kw a manispaa hiyo baada ya kuona watoto wao wanakaa chini kwa kukosa madawati; https://youtu.be/d711hM5YdNE
  
SIMU.tv: Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wametoa shukrani zao kwa serikali kwa kuanzisha usafiri wa mabasi yaendayo kasi baada ya kurahisha  shuguhuli zao mbalimbali jijini hapo; https://youtu.be/3rnPpImY2VE

SIMU.tv: Baadhi ya madereva wanaoendesha mabasi ya umma jijini Dar es salaam wapongeza matumizi ya Daraja la Nyerere Kigamboni huku wakiomba serikali kuweka malipo ya awamu ili kuwarahisishia shughuli zao;https://youtu.be/WfZGeZ1rTdo

SIMU.tv: Rais mstaafu wa awamu ya pili Mh Alli Hassan Mwinyi amesema jukumu la kuwalea na kuwatunza wazee ni la kila mmoja wetu hivyo kila mmoja kwa nafasia anapaswa kuwahudumia wasiojiweza; https://youtu.be/r12sk3EadR8

SIMU.tv: Bondia Mtanzania Thomas Mashali amefanikiwa kumtwanga  bondia kutoka nchini Iran kwa pointi na kufanikiwa kunyakua ubingwa wa dunia wa UBO; https://youtu.be/3hOuu8bVrzw

SIMU.tv: Timu ya soka ya Yanga imekabidhiwa kikombe chake  hapo jana katika mchezo wao na Ndanda baada ya kutoka kwa sare ya mabao 2 kwa 2; https://youtu.be/ua811XOJJvY

SIMU.tv: Timu ya kikapu Oilers ya Dar es salaam yaifunga timu ya Young Warriors  kutoka Morogoro na kujiweka katika nafasi nzuri ya kunyakua kikombe; https://youtu.be/AIUqxxw_xFU
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA