HII NDO RAMANI SAHIHI YA TANZANIA, KITENDO CHA KUCHAPISHA RAMANI YA TANZANIA ISIYO RASMI NI KOSA KWA MUJIBU WA MAMLAKA


WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebaini kuwepo kwa ongezeko la matumizi ya ramani ya Tanzania ambayo mipaka yake imepotoshwa.
Upotoshwaji huu umefanywa kwenye “diary” (vitabu vya kumbukumbu na matukio), Kalenda, mabango, matangazo ya kwenye vyombo vya habari na sehemu nyinginezo. Jambo hilo la kupotosha mipaka ni hatari kwa usalama wa nchi.Ili kuepusha upotoshaji wa mipaka ya nchi yetu tunashauri ramani sahihi zitumike.Ramani sahihi ya Tanzania inatakiwa kuonesha mpaka kwa sehemu ya maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa ukipita katikati ya maziwa hayo. 
Hivi karibuni tumebaini matumizi ya ramani ya Tanzania  kwenye majarida, magazeti na hata Luninga inayopotosha mpaka kwa sehemu ya ziwa Nyasa ikionesha mpaka kupita pembezoni mwa ziwa.
Kitendo cha kuchapisha ramani yenye makosa kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi ni kosa kwa mujibu wa mamlaka (Instrument) ya Mhe. Waziri aliyepewa dhamana ya kusimamia sekta ya ardhi ikiwemo masuala ya upimaji na ramani.
Idara ya Upimaji na Ramani ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuandaa, kuchapisha, kutunza na kusambaza ramani zote nchini ipo tayari kutoa ramani kwa matumizi yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na ushauri kuhusu usahihi wa ramani kabla ya kuitumia.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.