4x4

LEICESTER CITY YAKABIDHIWA KOMBE LAO LA LIGI KUU ENGLAND Leicester City wamesherekea ubingwa wao wa Premier League ambao ni wa kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 132 iliyopita.
Furaha hiyo imechagizwa na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa King Power.
Leicester wamekabidhiwa rasmi ubingwa wao baada ya kujihakikishia kutwaa taji hilo tangu siku ya Jumatatu wakati Tottenham iliposhindwa kuifunga Chelsea.
Klabu hiyo imeandika historia ambayo imeuteka ulimwengu ambapo nahodha Wes Morgan pamoja na kocha Claudia Ranieri kwa pamoja walinyanyua taji la Premier League baada ya kumaliza safari ya kupambana kutoshuka daraja hadi kutwaa ubingwa katika kipindi cha miezi 12.
Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton ulikuwa unaendelea kudhihirisha uwezo, kujitoa na ubora uliowapa ubingwa, lakini siku ya Jumamosi ya May 7 ni zaidi ya mchezo wa soka kutokana na kufunikwa na hisia za kila aina.


Post a Comment