MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano  la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016



 Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI