MBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI,JAFARY MICHAEL ATEMBELEA KATA ZILIZOATHIRIKA NA MVUA ZILIZONYESHA HIVI KARIBUNI


Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael (mwenye suti) akiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya (Kulia) wakizungumza na Diwani wa kata ya Ng'ambo ,Genesis Kiwhelu walipofika katika kata hiyo kujionea athari za miondombinu iliyotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Sehemu ya miondo mbunu ya maji ikiwa imeharibika.
Mbuge Jafary Michael na Mstahiki Meya ,Raymond Mboya pamoja na Diwani wa kata ya Ng'ambo Genesis Kiwhelu wakiangalia eneo la daraja lililopo katka kata hiyo namna lilivyoharibika kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Sehemu ya daraja hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akiwa katika moja ya kivuko kilichopo kata ya Ng'ambo akiangalia athari ya mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Diwani wa kata ya Msaranga,Anna Mushi akimueleza jambo Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael alipofanya ziara ya kujionea athari ya mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuharibu miundombinu.
Sehemu ya Korongo lililopo katika kati hiyo lililotokana na mvua .
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akisaidia kupalia mahindi wakati akiwa katika kata ya Msaranga akitembelea kujionea athari ya mvua iliyosababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akisadia kaika palizi la Mahindi katika moja ya shamba lililopo kata ya Msaranga.
Diwani wa kata ya Mji Mpya Abuu Shayo akimueleza jambo Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafaryy Michael alipofika katika kata hiyo kujionea athari ya mvua iliyosababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu .
Diwani wa kata ya Njoro ,Jomba John Koi akionesha sehemu ya uharibifu uliotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuharibu miundombinu.
Sehemu ya Miundombinu ikiwa imeharibika vibaya.
Taka zikiwa zimekwama katika moja ya daraja na kusababisha maji kushindwa kupita vizuri.
Diwani wa kata ya Njoro Jomba Koi akionesha sehemu ya mto Njoro ambao unategemewa kupitisha maji .
Mto Njoro kama unavyoonekana baada ya shughuli za kibinadamu kufanyika.
Ukuta ukiwa umeanguka kutokana na kupitiwa na maji.
Sehemu ya Miundombinu ikiwa imezidiwa na maji ,hatimaye maji yakatafuta njia ambayo iko jirani kabisa na makazi ya watu katika kata ya Njoro.
Hii ndio hali ilivyokuwa kutokana na Mvua hizo.
Sehemu ya Korongo ambalo limekuwa likipitisha maji katika kata ya Pasua eneo la Matindigani.
Diwani wa kata ya Pasua ,Charles Mkalakala akionesha sehemu ambayo uharibifu wa miundombinu ilivyoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akitizama eneo la karavati linalotumika kutisha maji likiwa limeziba.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*