MGENI AKATAA KUKANYAGA PEKU ZURIA 'CHAFU' BUNGENI

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MGENI mmoja mwalikwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Shamim (pichani kushoto) amekataa kuvua viatu akidai hawezi kukanyaga zuria chafu lililotandikwa katika mashine za ukaguzi bungeni, Dodoma.

Tukio hilo lilitokea jana asubuhi wakati Shamim akikaguliwa kwenye mashine hizo za ukaguzi na kengere kulia ambapo maofisa usalama wa Bunge waligundua kuwa viatu vyake vina matatizo hivyo kumwamuru avue.

Shamim alionekana kuwajia juu maofisa hao na kuwaambia kuwa hawezi kuvua viatu na kusisitiza kwamba miguu yake haiwezi kukanyaka zuria lililochafuliwa na watu ambao hawajulikani walikotoka.

Maofisa usalama walimweleza kuwa iwe isiwe lazima afuate utaratibu avue viatu ndiyo aruhusiwe kupita au arudi alikotoka.

Alielezwa kuwa endapo kama anaona anaonewa basi ruhusa kwenda kwa Katibu wa Bunge, akatoe malalamiko yake, lakini sheria na taratibu za hapo lazima zifuate.

Licha ya kuambiwa hivyo, Shamim alionekana kushindwa na kutaka kulazimisha kupita huku akilalamika kuwa hawezi kupita pekupeku ili hali anajua anaweza kupata magonjwa ya kuambukizwa yakiwemo ya ngozi.

Baada ya kuona maofisa hao wameshikilia msimamo wao, Shamim alivua viatu kwa hasira na kupita kwenye mashine huku akitoa lugha chafu iliyowaudhi maofisa hao.

Mmoja wa wabunge wanawake aliyeshuhudia sakata hilo, alimsihi Shamim kuacha maneno hayo ya maudhi na kumueleza kuwa hata wabunge wanafuata utaratibu huo sikwa wageni tu. Alimweleza kuwa siku moja alizuiwa kuingia bungeni baada kengere kulia na kugundua kuwa katika hijab aliyofaa kulikuwa na kibanio cha chuma na alikitoa.

Mbunge huyo aliwaomba maofisa usalama kumsamehe Shamim wamruhusu aingie bungeni, akaruhusiwa lakini baada ya kukubali kuvua viatu na kupita pekupeku kwenye zuria hilo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND