MUFTI WA TANZANIA ALAANI KITENDO CHA MAUAJI YALIYOTOKEA MKOANI MWANZA.



 Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir (Mwenye kofia Nyeupe katikati) akiwa na viongozi mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

SHEKHE Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir pamoja amelaani vikali tukio la kinyama lililotokea Mei 17 mwaka huu katika Msikiti wa Ibanda Mkolani, Masjid Rahmaan mkoani Mwanza. 

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa  kitendo hicho kuwa ni cha kinyama na hakivumiliki.

Tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu na kusababisha mauaji ya waumini watatu wa Msikiti wa Ibanda Mkolani waliokuwa katika Ibada  miongoni mwao akiwa ni Imam wa Msikiti huo ikiwa na wengine kujeruhiwa.

"Kwaniaba ya Baraza kuu la Waislam wa Tanzania(Bakwata) tunalaani vikali tukio hili pamoja na kuwataka Waislam wawe watulivu katika kipindi hiki kigumu" Amesema Shekhe Zuberi.

Amewaomba Waislam na wananchi kwa ujumla kuvipa ushirikiano wa hali na mali vyombo vya usalam ili hatimae kuwapata waharifu hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria.



Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, na kulaani kitendo cha mauaji ya watu wasio na hatia katika Msikiti huko Mkoani Mwanza. Kulia ni Msaidizi katika ofisi ya Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe, Ally Khamisi Ngeruko. na Kushoto ni Shekhe, Abuubakari Kharid.
Baadhi ya waamini wa dini ya Kiislamu pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Shekhe Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mufti wa Tanzania, Aboubakar Zubeir jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA