MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN PAMOJA NA MKUU WA MAJESHI MWAMUNYAGE



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza,Arusha
Jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia mwanafunzi wa  Mwaka wa tatu  wa chuo cha maendeleo  ya jamii .Tengeru  aliyejulikana kwa jina la  Harold Mmbando (23)  mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis  Mwamunyange  pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.Akiongelea  tukio kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo  alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 17 mwaka huu majira ya saa 09:00  asubuhi .Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi  ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe  nje ya nchi huku hakuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.
“mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtuhumiwa huyo  alisambaza ujumbe  mwingine wenye maneno yafuatayo,”Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida”hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia  mitandao ya kijamii kama faccebook.

Mkumbo  alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa  rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo  ya kijamii pasipo kukiuka sheria  na taratiu za kisheria .Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika  anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa  atachukuliwa hatuakali za kisheria  dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa  wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  John Pombe Magufuli Isaac Emily (40),  mkazi wa Olasiti jiji  hapa  inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.