SERA YA TEHAMA YA 2016 KUSAIDIA TANZANIA KUINGIA KATIKA UCHUMI WA KATI MWAKA 2025.


index
Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dodoma.
 
Serikali kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya Nchi wameifanyia maboresho Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2003  na kuja ya sera mpya ya mwaka 2016 ili kuunganisha sekta muhimu za uzalishaji na viwanda katika miundombinu ya TEHAMA.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Sera ya Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano ya mwaka 2016.
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania kutumia fursa zinatokana na uwepo wa miundombinu ya TEHAMA kuingia katika uchumi wa kati ifakapo 2025 kwa kuimarisha matumizi ya TEHAMa katika sekta mbalimbali za uzalishaji nchini.
Mhe. Ngonyani aliongeza kuwa Sera hiyo ni muhimu katika kujenga jamii habari itakayowezesha nchi kufikia maarifa yatakayosaidia kwenda sanajari na mpango wa Taifa kujenga uchumi wa viwanda.
Alisema kuwa Sera hiyo imejikita katika kukuza matumzi TEHAMA katika uzalishaji ili kuongeza tija , kukuza utafiti na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika TEHAMA kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
 Awali akiongea kabla ya uzinduzi wa Sera hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano(Mawasiliano)  Profesa Faustin Kamuzora alisema kuwa Sera hiyo itasaidia kuongeza ufanisi wa utendaji wa kazi wa kila siku katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema kuwa sera hii itasiaidia kwenda sanajari ya ukuaji wa kasi wa matumzi ya mawasiliano hapa nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*