SERIKALI YABORESHA SEKTA YA HALI YA HEWA NA KUFIKIA YA KIWANGO CHA KIMATAIFA.

HALINa Anitha Jonas – MAELEZO.
“Wahenga wanasema penye nia pana njia na haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo.” Hatimae Serikali imetimiza ndoto zake za kuwa na kituo bora chenye kutoa  taarifa za uhakika zinazohusu masuala ya hali ya hewa katika kiwango cha Kimataifa.
Serikali imeweza kufanikisha hili kwa kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuboresha huduma hizo kwa asilimia 80. Haya ni mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba kufahamu habari za hali ya hewa kunasaidia sana kupanga shughuli za kiuchumi na maendeleo.
Hilo limejidhihirisha hivi karibuni katika taarifa ya tahadhari kuwepo kwa mvua zitakazo ambatana na upepo kutokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua sambamba na uwepo wa kimbunga Fantala katika Bahari ya Hindi.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dkt. Agness Kijazi na kusema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Aprili 13-16,2016 ambapo kutakuwa na mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24. na hili limetokea kama lilivyotabiriwa. Wenye kuchukua tahadhari wamesha hivyo na kuepuka madhara yatokanayo na mafuriko. Waliohama baadhi ya sehemu za mabondeni, walishukuru baada ya kuona makazi yao ya awali yakifunikwa kabisa na maji.
Mvua hizo zilikuwa zikiathiri mkoa wa Tanga, Dar es Salaam, Pwani,Morogoro pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Kuthibitisha kuwa kituo hicho kinatoa taarifa za uhakika ni pale ambapo mwaka jana Dkt. Agness Kijazi alitangaza kuwepo na mvua za EL-NINO kuanzia mwanzoni mwa mwezi Septemba–Desemba 2015. Hii ilithibitika baada kushuhudia kuwepo kwa mvua hizo katika maeneo mbali mbali ya nchi ambapo        mvua hizo zilisababisha mafuriko na uharibifu wa miundombinu,makazi na mazao ya wakulima.
Utabiri huo wa kuaminika unatokana na TMA kuboresha mtandao wa vituo na usimikaji wa mitambo ya hali ya hewa pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya hali ya hewa ambapo vituo vitatu vyenye mitambo ya kisasa vimejengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kilwa Masoko- Lindi, Mpanda-Katavi na Songwe.Vituo hivi vimechangia kuongeza upatikanaji wa takwimu na taarifa za hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi nchini.
Kwa sasaSerikali kupitia TMA imeanzisha kituo cha kupimia hali ya hewa na Kilimo kiitwacho Agromet Station hukoMatangutuani Pemba na hivyo kuongeza idadi ya vituo vya kutoa huduma za hali ya hewa katika sekta ya Kilimo na kufikia vituo 15 nchini,hivyo kuongeza ubora wa taarifa zinazotolewa.
Kwa upande wa taarifa za anga ya juu Mamlaka imeimarisha huduma za Usafiri wa Anga kwa kuboresha mtambo wa kupima hali ya hewa katika anga za juu (Modernization of Upper Air System) katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) pamoja na kufufua kituo cha kupima taarifa za anga ya juu kilichopoTabora.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI