UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE, (JNIA), WAPATA SHIRIKA LINGINE LA NDEGE, NI MAURITIUS AIRLINES


 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, akiielekeza ndege ya Shirika la
Ndege Mauritius Airlines, kuegesha kwenye daraja la kushukia abiria (Bridge),
kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mei6, 2016. Ndege hiyo aina ya Airbus 319 yenye uwezo wa kubeba abiria 130, imetuakwa mara ya kwanza na itakuwa ikifanya safari zake kila Ijumaa ikiruka moja kwamoja kutoka Mauritius kuja Dar es Salaam kasha Nairobi, nchini Kenya.
Magari ya zimamoto yakiipokea ndege hiyo kwa kuimwagia maji ikiwa ni ishara ya ukaribisho
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said, JNIA
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, kupitia uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere, imeongeza idadi ya mashirika ya ndege yanayotumia uwanja huo
baada ya ndege ya kwanza ya Shirika la Ndege la Mauritius (Mauritus Airlines),
kutua kwenye uwanja huo leo Mei 6, 2016.
Ndege
hiyo aina ya Boeng Airbus 319, yenye kubeba abiria 130, ilitua kwenye uwanja
huo majira ya saa 5;20 asubuhi ambapo kama ilivyoada ya kupokea ndege mpya
inayoanza shughuli zake kwenye uwanja huo, magari mawili ya zimamoto yalipiga
(saluti), kumwagilia maji ndege hiyo wakati ikielekea kuegesha kwenye daraja la
kushukia abiria.
Kwa
mujibu wa maafisa wa Shirika hilo, ndege hiyo itakuwa ikiruka kutoka Mauritius
moja kwa moja na kutua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
ambapo itashusha abiria na kuelekea 
uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
“Safari ya kutoka Mauritius kuja Dar es Slaam ni kiasi ya masaa matatu .”alisema rubani
mkuu wa ndege hiyo, Parikshant Nundlol
Maafisa wa TAA walisema  kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari yake mara
moja kwa wiki kila siku ya Ijumaa.
 Rubani mkuu wa ndege hiyo, Parikshany Nundlol, akizungumza na waandishi wa habari wa Mauritius waliofuatana na ndege hiyo
Warembo wa Kitanzania walioshiriki kuipokea ndege hiyo
Wafanyaakzi wa shirika la ndege la Mauritius na wale wa Swissport wakiwa katika picha ya pamoja
 Abiria wa kwanza waliowasili na ndege hiyo

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS