VYAMA VYA SIASA WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA KUTATUA MIGOGORO


MS1Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini Mhe. Peter Kuga Mziray akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam  . Kulia ni Mhe. Jaji Francis S.K Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa na Mhe. Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti wa Baraza .
MS3Bw. John Cheyo  mmoja wa wajumbe wa Baraza la vyama vya siasa akichangia hoja  wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
MS2Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam.
MS4Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
MS5Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakifuatilia mjadala wakati wa kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
MS6Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Baraza la vyama vya Siasa baada ya kikao cha Baraza kujadili Mapendekezo ya Mfumo wa utatuzi wa migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa GEPF Victoria Jijini Dar es salaam. 
………………………………………………………………………………………………………
Na Monica Laurent -Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini ambalo linaundwa na  wawakilishi wawili kutoka kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu wamekutana mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa GEPF uliopo Victoria Jijini Dar es salam kujadili mapendekezo ya mfumo wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama vya siasa .
Mapendekezo hayo yalitolewa na Mtaalamu wa utatuzi wa Migogoro Bw. Ghalib Galant ambaye awali alifanya utafiti wa utatuzi wa migogoro ya ndani na baina ya vyama  vya siasa  nchini chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  na kwa udhamini  wa UNDP  kupitia mradi wake wa “Democratic Project” ukiwa na lengo la kuiboresha sura namba 258 ya Sheria ya Vyama vya Siasa  ya mwaka 1992 ili kuendana na mahitaji ya ukuaji wa demokrasia nchini. Utafiti huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa demokrasia ya vyama vingi nchini vikiwemo vyama vya siasa.
Akiwasilisha mapendekezo, Msajili Msaidizi Bi. Piencia C. Kiure ,alisema kuwa  ilipendekezwa kuwa Sheria ya Vyama vya Siasa nchini iweke masharti yanayohusu utaratibu  wa kutatua migogoro ndani na baina ya vyama vya siasa “ migogoro  ndani ya chama ni lazima ishughulikiwe kwanza ndani ya chama cha siasa  na kufikia tamati kwa mfumo wa utatuzi wa migogoro uliowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, kabla ya kuwasilishwa katika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kwa ajili ya upatanishi” ilikaririwa  sehemu ya mapendekezo
“Upatanishi ukishindikana mgogoro husika uwasilishwe kwenye Baraza  la Uamuzi la Migogoro ya Vyama vya Siasa kwa uamuzi. Ikiwa muhusika wa mgogoro asiporidhika na uamuzi wa Baraza  la Uamuzi wa migogoro ya vyama vya siasa atawasilisha mgogoro husika Mahakama Kuu mbele ya Majaji watatu kwa mapitio ya uamuzi wa Baraza. Muhusika asiporidhika  na uamuzi wa Mahakama Kuu, atakata  rufaa Mahakama ya Rufaa” ilifafanua sehemu ya Mapendekezo.
Aidha kumekuwa na msisitizo wa kufuata mtiririko wa hatua katika utatuzi wa migogoro kama ilivyobainishwa hapo juu ili kuepusha migogoro ndani ya vyama  kwenda moja kwa moja  Mahakamani ambako huchukua muda mrefu  na kuathiri ukuaji wa demockaria ndani na nje ya vyama vya siasa hapa nchini.
Wakichangia katika mjadala huo, baadhi ya wajumbe walikubaliana na hoja kuwa  vyama vya siasa vitatue kwanza migogoro yake ndani ya vyama na kwamba pale tu itakaposhindikana ndipo ipelekwe kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Wajumbe walishindwa kukubaliana katika  hoja ya uwepo wa Baraza la Uamuzi  wa Migogoro ya vyama vya siasa, wapo walioona haja ya uwepo wake  na wapo walipendekeza kuwa majukumu ya Baraza hilo yafanywe na Baraza la Vyama vya siasa lililopo sasa jambo lililosababisha kutokukubaliana katika hoja hiyo.
Pamoja na michango iliyotolewa , Wajumbe wameishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwekeza katika Baraza la Vyama vya Siasa  ili kusaidia utatuzi wa migogoro nchini kwa kuwa imebainika kuwa machafuko katika nchi nyingi duniani yamesababishwa na machafuko katika masuala ya siasa.
Akihitaji ufafanuzi wa  hatua gani imefikiwa katika uboreshaji wa Sheria ya Vyama vya siasa, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, Mhe. Peter Kugar Mziray aliiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kutoa ufafanuzi. Naye Msajili Msaidizi, Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi alisema tayari vyama vyote vya siasa vimeshapelekewa barua vikiombwa kuwasilisha mapendekezo kwa ajili ya kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na kwamba Ofisi inafanya jitihada za kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau wa siasa na ikishakamilisha upokeaji huo, mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye kamati ya Katiba na Sheria.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI