WAJUMBE WA KAMATI YA MISS TANZANIA 2016/17 WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE KUPATA WAFADHILI WA MASHINDANO HAYO


mis1Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akiongea na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wakati wa kikao baina yao kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga. Picha na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
mis2Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 mara baada kumalizika kwa kikao  baina yao kilichofanyika   mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma.
mis3Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania, Lilian Kamazima  mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baadhi ya wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa TBC mjini Dodoma. Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
mis4Miss Tanzania, Lilian Kamazima  (kushoto) akimshukuru Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura kwa  kukubali kukutana na wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu. Kikao hicho kilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) uliopo mjini Dodoma.
………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Maalum  – Dodoma
 Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wameiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Ombi hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga wakati akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokutana nao mjini Dodoma.
Lundenga alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni kupata ufadhili wa mashindano hayo ambayo yanafaida kwa mabinti wanaoshiriki hii ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kuwa viongozi wazuri wa baadaye.
“Mwezi wa tisa warembo wanatarajiwa kuingia kambini watakaa huko kwa muda wa mwezi mmoja ambako watapewa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja kufundishwa jinsi ya  kujitambua na kujiendeleza kielimu”, alisema Lundenga.
Kwa upande wake Mhe. Wambura aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa kuandaa mashindano hayo na kuwaahidi kushirikiana nao ili  kuhakikisha mashindano yanafanyika kama ilivyotarajiwa.
Mhe. Wambura alisema, “Nawapongeza washiriki wa mashindano haya walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia kwani wameweza kushika nafasi nzuri katika mashindano ya makundi mbalimbali pia hawajawaangusha waandaaji wa mashindano kwa kuwa wanaendelea kuisaidia jamii inayowazunguka.
Naye Miss Tanzania,  Lilian Kamazima  alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukubali kukutana nao na kusema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa lisha ya washiriki kupewa zawadi mbalimbali  lakini pia   wakiwa katika maandalizi ya mashindano  wanafundishwa jinsi ya kuwa wanawake wa kuigwa katika jamii, kuishi na kuisaidia jamii inayowazunguka.
Mashindano ya Miss Tanzania Taifa yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, hivi sasa mashindano ya vitongoji (Vituo) yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini baada ya hapo yatafuatiwa na mashindano ya Kanda.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.