WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO YALAANI MAUAJI YA MTOTO SARA MGIMBA (14)


logoWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inalaani tukio la kubakwa na kuuawa kwa mtoto Sara Mgimba (14), mkazi wa kijiji cha Lugarawa, wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe ambaye mwili wake uliokotwa mto Lugarawa, siku ya tarehe 18/5/2016.Wizara imesikitishwa na taarifa ya kifo cha mtoto Sara, ambaye mwilini wake ulioopolewa mtoni akiwa alitobolewa macho, mwilini akiwa mtupu; jambo linaloashiria kuwa marehemu alibakwa kabla ya mauti kumfika. Inaelezwa kuwa, alifungwa kanga shingoni, na kufungiwa ndani ya sandarusi mbili (2) zenye mawe, na kuzamishwa mto Lugarawa, hadi Uongozi wa kijiji cha Lugarawa walipoopoa mwili wake majini wakati walipoendesha msako, mapema wiki hii.  Wizara inapongeza juhudi za wanakijiji na jeshi la Polisi katika mkoa wa Njombe ambao walifika sehemu ya tukio ili kufuatilia mauaji hayo. Ni imani ya Wizara ya watoto kuwa, Polisi kwa kutumia weledi wao na kwa kushirikiana na wananchi wataweza kuwakamata watuhumiwa wa mauaji hayo na kuwachukulia hatua stahiki.Wizara inasisitiza kwamba  kila binadamu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa Sheria za nchi. Vitendo vya ubakaji na maujai ya kikatili vinapotokea katika familia zetu vinadhohofisha juhudi za wananchi katika kujiletea maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi, hivyo ni muhimu kuzuia na kutokomeza aina zote za ukatili kwa watoto.
Wizara inaomba wanafamilia waliopatwa na msiba huu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa, wakati Polisi wakiendelea kuwasaka watuhumiwa wa mauaji hayo.
                       Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
                      Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
                          15/4/2016

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA