DC BAGAMOYO AMTUMBUA MWEKEZAJI MKOREA KWA KUMPOKONYA ARDHI NA KUIRUDISHA KWA WANANCHI


indexMkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Majid Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha mwavi kata ta Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mkutano maalumu na kutatua sakata la mgogoro wa ardhi baina yao pamoja na mwekezaji Mkorea, ambaye amepokonywa hekari 131 na zimerudishwa kwa wananchi wenyewe.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
index1Baadhi ya wawekezaji hao ambao ni wakorea wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo.
…………………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi  kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua  kuliingilia kati  suala hilo kwa lego la  kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti zilizokuwepo.
Mgogoro huo ambao umeonekana kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo.
Akizungumzia kuhusina na sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga  alisema kwamba baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu.
“Jamani wananchi wa kijiji cha  mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama tulivyokubaliana.
Alisema kwamba  serikali ya awamu ya tano ambayo inangozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli itahakikisha kwamba inaleta mabadiliko chanya kwa kuzingatia usawa bila ya kuwa na uonevu wowote ule hasa katika masuala ya ardhi ambayo yameonekana kuwa ni changamoto kubwa katika Wilaya ya bagamoyo na maeneo mengine, na kuahidi kushirikiana nao mambo yote ya kimaendeleo.
Aidha amepiga marufuku kwa wenyekiti wa vijiji na vitongoji vyote kutouza ardhi kiholela bila ya kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na badala yake tabia hiyo waiche mara moja vinginevyo atawachukulia hataua kali za kisheri ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
“Hii tabia ya watendaji wetu kufanya jambo la kuuza ardhi bila kuzingatia sheria ni baya sana na ndio maana linatufukisha  katika hatua kama hii ya kugombania ardhi na kusababisha migogoro sasa sitaki kuona hali hiyo, kwani huna mamlaka yoyote ya kuuza ardhi hata mita mbili kwa hiyo naomba hili lizingatiwe sitaki kuona migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Bagamoyo, alisema Mwanga.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho akiwemo Ramadhani Mfaume,Salum Hamad,Kulwa Ramadhani pamoja na Semeni Manga wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo wamesema kwamba walikuwa wanashindwa kufanya shughuli zozote za kimaendeleo kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo wa ardhi baina yao na mwekezaji huyo.
Walisema kwamba mwekezaji huyo alipewa eneo hilo tangu mwaka 1997 na baadhi ya watendaji wa kijiji  kwa ajili ya uwekezaji lakini wanashangaa ameshindwa kuliendeleza kitu ambacho waliamua kwenda kutoa kilio chao kwa mkuu wa Wilaya kuhusiana na hekali hizo ambapo wanashukuru ameweza kulishughulikia suala hilo na kufanikiwa kuzirudisha hekari 131 za kijiji.
“Kwa weli sisi kama wananchi wa kijiji cha mwavi tulikuwa katika hali ya mvutano mkubwa wa siku nyine na mwekezaji huyo ambaye ni mkorea, juu ya kutuchukulia ardhi yetu lakini tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wetu wa Wilaya kuweza kulitatua suala hilo ambalo lilikuwa inatumbumbua kwa muda mrefu, walisema wanakijiji hao.
Pia waliongeza kuwa kurudishwa  kwa hekari  hizo 131 zitaweza kuwapa fursa ya kuweza kufanya shughuli mbali za kimaendeleo ikiwemo kujenga ujenzi wa shule kwa ajili ya watoto wao,masoko, pamoja na zahanati kwani hapo awali walikuwa hawana huduma za karibu katika kijiji hicho.
Pia mwandishi wa habari hizi iliweza kupata fursa ya kuzungumza na mmwekezaji huyo ambaye ni Mkorea anayejulikana kwa jina la Yum Yun Hwa ambapo alisema kwamba lengo lake kubwa la kuchukua eneo hilo ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa eneo hilo kwa kuweka viwanda, shule, zahanati pamoja na kuanzsiha kituo maalumu cha kilimo.
Yum hwa alibainisha kwamba katika kuunga juhudi za serikali ya Tanzania katika kuendeeza kilimo cha kisasa amepanga kuwaleta wataalamu kutoka nchini korea ambapo watakuja katika kituo hicho kwa ajili ya kufundisha  masuala mbali mbali ya kilimo, na kuongeza kuwa tayari wameshafanya ununuzi wa vifaa ikiwemo matrekta,Power tila ambayo yatakuwa kwa ajili ya shughuli za kilimo.
 Kijiji hicho cha mwavi kilichopo kata ya Fukayosi Wilayani Bagamoyo kiliingia katika mgogoro wa ardhi na mwekezaji huyo tangu mwaka 1997, ambapo kutokana na juhudi zilizofanywa na  Mkuu wa Wiaya ya Bgamoyo kuamua kuingilia katia sakata hili kumeweza kusaidia kutokana na mwekezaji huyo kukubali kuwarudhishia ardhi yao wananchi yenye ukumbwa wa hekari 131.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI