KAMPUNI YA ASAS DAIRIES LTD YASHINDA TENA TUZO YA UBORA

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo akimkabidhi meneja uzalishaji wa kampuni ya  Asas Dairies Ltd Bw Lipita  Mtimila tuzo baada ya  kampuni yake  kushinda  tuzo ya  ubora katika maonyesho ya  wiki ya Maziwa Nchini
Tuzo  ya  Ushindi  ya mwaka 2016
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo akitembelea  banda  la kampuni ya  Asas dairies Ltd
Viongozi  wakitazama bidhaa za  kampuni ya  Asas
Wanafunzi  wakiwa katika  picha ya  pamoja  katika  maonyesho ya   wiki ya Maziwa
Meneja  uzalishaji  wa kampuni ya  Asas Dairies Ltd Bw Lipita Mtimila akionyesha cheti  cha  ushindi wa jumla  ambacho kampuni   hiyo  ilikabidhiwa
Bw  Mtimila akionyesha  vyeti  vya  ushindi wa  uzalishaji  wa bidhaa bora
Vyeti vya  ushindi 
                            Na Matukiodaima Blog                  

KAMPUNI  ya Asas Dairies Ltd ya  mkoani Iringa kwa mara ya nne mfululizo imeendelea kushika nafasi ya  kwanza kitaifa   uzalishaji wa maziwa nchini . 

Kampuni  hiyo imeshinda tuzo  ya wazalishaji wakubwa wa bidhaa bora  za maziwa  katika mashindano   wiki ya maziwa yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya  shule ya sekondari Mpechi mkoani Njombe .

Kampuni  hiyo imeibuka  mshindi  wa  kwanza  baada ya  kuongoza  katika nafasi zote  tatu  za  ubora  wa  bidhaa zilizoshindanishwa  katika mashindano  hayo .

Akikabidhi tuzo hizo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi  Dkt. Mary Mashingo pamoja na kupongeza makampuni yaliyoshiriki katika zoezi hilo bado alipongeza  kampuni   ya Asas Dairies  Ltd  kwa   kufanya  vizuri katika mashindano hayo ya ubora  wa maziwa nchini 
Alisema  kuwa jitihada  zilizoonyeshwa na kampuni  hiyo ni kubwa na  zinapaswa  kuigwa na makampuni mengine hapa nchini.

Kwani  alisema  kuwa  kuongoza katika nafasi zote zilizoshindaniwa si  jambo dogo ni  jitihada  kubwa zimefanyika na ni hatua ya kujivunia kwa kampuni hiyo.


Pia     aliipongeza  bodi ya maziwa Tanzania kwa  kuandaa mashindano kama hayo kwani ni sehemu ya  kipimo kwa  wamiliki wa  viwanda vya maziwa  nchini na sehemu  ya  kujitathimini  .


Kwa upande  wake  meneja  uzalishaji  wa kampuni hiyo ya Asas Dairies Ltd  Lipita Mtimila   alisema kuwa mbali ya kampuni  hiyo kuongoza kwa mwaka  huu bado  ilipata  kuongoza katika mashinadano kama haya  miaka  mitatu  nyuma  na  hii ni mara ya nne  kuongoza .

Katika mashindano hayo  yaliyoandaliwa na bodi ya maziwa  Tanzania( TDB)  kampuni ya Asas Dairies iliweza  kuibuka na ushindi  wa  jumla baada ya kushinda tuzo zote  tatu  dhidi ya makapuni  mengine  ya uzalishaji maziwa  yaliyoshiriki katika mashindano hayo .

Bw Mtimila aliwataka  watanzania kuendelea  kuzipenda  bidhaa za Asas Dairies Ltd  na  kuwa  lengo la kampuni  hiyo ni kuendelea  kuzalishaji bidhaa zenye  ubora zaidi .

Pia  alipongeza watanzania na watumiaji wa bidhaa za Asas Dairies Ltd kutokana na ushirikiano mkubwa  wanaoutoa kwa  kuendelea  kutumia maziwa yanayozalishwa na kampuni  hiyo ya Asas Dairies Ltd Iringa

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.

YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

KWA HERI KAMANDA WETU ABBAS KANDORO