LWENGE ATAKA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI WASHTAKIWE KWA KOSA LA UHUJU UCHUMI

indexWaziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua koki ya maji katika mradi wa maji wa Chiruku Wilayani Chemba. nyuma ni Mbunge wa Chemba Alhaji Juma Nkamia.
index1Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Lwenge akimtwisha ndoo ya maji Rawiya Hassani mkazi wa Chiruku.
index3Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Lwenge akikagua moja ya matanki ya maji katika mradi wa maji wa Ntomoko Wilayani Chemba.
index5Waziri wa Maji na Umwagiliaji akiongea na wakazi wa Itolwa Wilayani Chemba kabla ya kuhitimisha ziara yake katika wilaya hiyo.
………………………………………………………………………………………………………
Na Athumani Shariff;
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge ametaka watendaji wa Halmashauri nchini kuwashtaki watu wanaohujumu miundombinu ya maji kama wahujumu uchumi.
Hayo aliyasema leo alipofanya ziara katika kijiji cha Bumila kata ya Lupeta  Halmashauri ya Mpwapwa baada ya kupokea taarifa ya hali ya huduma ya maji katika kijiji hicho.
“Naagiza Halmashauri muwatafute watu wote waliohujumu miundombinu ya maji na washitakiwe kama wahujumu uchumi, hatuwezi kuwaachia watu wanaosababisha wananchi wasio na hatia kukosa huduma muhimu ya maji”
Miundombinu ya maji katika kijiji cha Bumila imehujumiwa kwa mabomba zaidi ya 40 ya nchi 2 yenye urefu wa mita 6 kwa kila kipande cha bomba kung’olewa na hatimaye maji kutokuwafikia wananchi. 
Katika hali ya kulikabili tatizo la maji katika kijiji hicho Mhandisi Lwenge ameiagiza Halmashauri ya Mpwapwa kuchimba kisima katika kijiji cha Bumila haraka ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji hicho.
Katika hatua nyingine Waziri Lwenge amewataka viongozi na watendaji wote nchini kushughulikia maswala ya maji badala ya kuachiwa yeye Waziri wa Maji peke yake.
 “Kila mmoja wetu kwa nafasi yake ana jukumu la kufatilia maswala haya sio ya waziri wa maji peke yake, Wilayani mkishindwa mpeleke Mkoani nao wakishindwa wataleta Wizarani nasi tukishindwa tutapeleka kwa Magufuli kitu ambacho sitegemei” Alisema Waziri Lwenge.
Akiwa Wilayani Chemba, Waziri Lwenge amekataza tabia ya baadhi ya vijiji, kata na jamii za watu wanao wabagua jamii nyingine katika miradi ya maji. Akiwa wilayani humo Lwenge aliagiza kuwa miradi yote ya maji ni mali ya serikali hivyo jamii zote bila kujali mipaka ya kijiografia kupata huduma hiyo.
“Maji yote ni mali ya serikali, hamna mtu wala kikundi cha mtu chenye kumiliki maji, hivyo hairuhusiwi kwa mtu au kikundi cha watu kujimilikisha maji na kubagua baadhi ya jamii ya watu wengine wasipate maj, sisi sote ni watanzania”. Alisema Waziri Lwenge.
Ziara ya Waziri Lwenge ilianza katika Halmashauri za Chemba na Kondoa na kuishia katika halmashauri ya Mpwapwa ikiwa ni ahadi aliyoitoa bungeni kwa mbunge wa Chemba Juma Nkamia na Mpwapwa George Lubeleje.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU