MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAUPONGEZA MGODI WA BUZWAGI.


  Meneja Uendelevu wa Mgodi wa Buzwagi, George Mkanza akifafanua jambo kwa madiwani wa halmshauri ya mji wa Kahama wakati ziara ya kutembelea Mgodi huo.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abel Shija(mwenye skafu) pamoja na waheshimiwa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wataalamu wa Mgodi huo.
  Afisa mazingira wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Lusajo Njobelo akifafanua jambo kwa waheshimiwa madiwani na mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba wakati wa ziara hiyo.
  Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Marco Peter katika eneo la uchimbaji.
  Shimo ambalo shughuli za uchimbaji hufanyika kama linavyoonekana.
   Eneo maalumu la kusagia mawe kabla ya kupelekwa kiwandani kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu.
Madiwani pamoja na wataalamu kutoka halmashauri ya mji wa Kahama wakipiga picha mbele ya moja ya mitambo inayotumika kusomba mawe mgodini hapo.
  Meneja Uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi Rodney Burgess (wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama.
  Wataalamu wa halmashauri ya mji wa Kahama wakiwa katika kituo cha kupozea umeme, kituo ambacho kinaelezwa kuwa kitatumika pia kufunga kifaa maalumu kilichonunuliwa na Mgodi wa Buzwagi ambacho kitawawezesha wananchi wa Kahama na viunga vyake kuweza kupata umeme wa uhakika.
  Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Magesa Magesa akiteta jambo na Katibu wa Mbunge wa Kahama mjini, Abdul Mpei wakati wa ziara ya madiwani ambayo pia ilihusisha wataalamu kutoka halmashauri.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza na madiwani wa halmashauri ya Kahama wakati wa kuhitimisha ziara yao walipotembelea Mgodi huo.
  Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba (Kulia) akiwa na mwenyekiti wa ya wilaya ya Kahama, Abeli Shija wakimsikiliza Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi wakati alipokuwa anazungumza na madiwani baada ya ziara yao.
  Picha ya pamoja baina ya madiwani wa Halmashauri ya mji wa Kahama, wataalamu wa halmashauri hiyo pamoja na maofisa wa Mgodi wa Buzwagi.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.


Madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa namna ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.



Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya siku moja iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za uchimbaji.

 

“Kwa niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna ambavyo mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika kwa sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo mbinu mlioiweka katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za kisasa ” alisema Shija.



Mwenyekiti huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha upatikanaji wa kifaa kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa uhakika ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa Kahama kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi wa mji wa huo.

 

Akijibu ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na kukifunga.

 

“Kifaa kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu kuja na kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa uhakika.” Alisema Mwaipopo.

 

Ziara hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa Kahama mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo, walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za mazingira na uchimbaji na  kulifanya eneo hilo kuwa salama zaidi.

Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza ufahamu kwa Jamii kwa kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa kawaida kwa lengo la kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali ambayo wamesema itasaidia kupunguza taarifa za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani kutokana na Jamii kutokujua ukweli.



Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA