MASAUNI ALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI MWANZA, ATOA RAMBIRAMBI KWA WAKE WA WALIOUAWA MSIKITINI


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa.
Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI