MBUNGE ROSE TWEVE AKERWA NA KINACHOENDELEA MSITU WA SAO HILL




Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM) Mkoa wa Iringa, akichangia bungeni Dodoma hivi karibuni, ambapo alielezea masikitiko yake kuhusu wawekezaji wanavyopewa kipaumbele kupata vibali vya bei poa kuliko wazawa katika Msitu wa Sao Hill uliopo wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Tweve aliitaka serikali kupunguza cubic meter 250,000  kati ya 600,000 wanazopewa wawekezaji ili zigawiwe kwa makundi ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu ili nao waonje matunda ya msitu wao huo.

Pia aliitaka serikali kuwapandishia  wawekezaji bei ya cubic  meter ambayo ni sh. 14,000 ili nao walipe sawa na wazawa'
 wanaolipishwa sh 28,000.

Alisema kawaida wazawa ambao ndiyo waliopanda miti na kuutunza msitu huo hivyo ndiyo wanaotakiwa kupewa kipaumbele kuliko wawekezaji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*