MKAPA AWATAKA WATANZANIA KUFANYA KAZI KWA BIDII.



Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa akikata utepe kuzindua kitabu cha kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala. 
Mwenyekiti wa Kitaifa wa chama cha ACT wazalendo Bi. Anna Mghwira akichangia hoja wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Mstaafu awamu ya tatu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Benjamin William Mkapa hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa nane wa kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika jijini Dar es salaam.Picha na Ally Daud-Maelezo

Na Ally Daud- Maelezo

Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali baada ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Dkt Mkapa.

Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwal. J.k nyerere. Mbali na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa madiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.

Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umeudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndan na nje ya nchi.

Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.Mbali na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI