4x4

ROSE TWEVE AKICHANGIA MAMBO MUHIMU BAJETI YA SERIKALI

 Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM)  Mkoa wa Iringa, alikuwa ni mmoja wa wabunge waliobahatika kuchangia mjadala wa Bajeti ya Serikali bungeni Dodoma, ambapo alitoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iweke mkakati maalumu wa kukusanya kodi kwenye halmashauri na aliiomba halmashauri ya Iringa itoe ushirikano kwani haina uwezo wa wafanyakazi wenye uwezo wa kukusanya kodi hizo.

Pia alitoa ombi kwa serikali ili ipeleke fedha hizo kwenye halmashauri kwa ajili ya maendeleo. 
Vile vile alikemea ubadhirifu mkubwa katika halmashauri hizo kwa wakatina kwa bajeti iliyotengwa..

Aidha aliitaka serikali kuipatia fedha za kutosha ofisi ya CAG kwani ni macho na masikio ya serikali yetu ili kudhibiti matumizi ya fedha zilizotengwa. 

Vilevile aliikumbusha serikali kuhusu changamoto ya afya na maji hasa katika hospitali/Zahanati  ambayo ni kero kubwa kiasi  kwamba vifo vya watoto na akina mama.


Post a Comment