SERIKALI KUANZA KUTAFITI MAJI YA MTO RUFIJI KATIKA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Na Ismail Ngayonga MAELEZO- Dodoma
……………………….
SERIKALI imesema katika mwaka wa fedha 2016/17 itaanza shughuli za utafiti wa maji ya mto rufiji ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa maji katika wilaya za mkoa huo na mkoa wa Dar es Salaam.
Akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Pwani, Hawa Mchafu, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  alisema mbali na utafiti huo, Serikali pia imekusudia kujenga bwawa la kidunda ili kuhakikisha kuwa  wakazi wa miji ya Pwani na Dar es Salaam wanakuwa na maji ya kutosha na yenye uhakika.
Alisema kwa sasa kuna vyanzo viwili vya maji ambavyo ni Ruvu Chini na Ruvu juu, hivyo kukamilika kwa mradi wa maji ya bwawa la kidunda itasaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji.
“Tayari mradi huu upo katika mpango wa Serikali ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 tayari Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 14 kwa ajili ya bwawa hilo” alisema Kamwelwe
Aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi wa Kidunda utasadia kwa kiasi kikubwa kutosheleza kwa maji katika vyanzo vya maji vya Ruvu juu na Ruvu chini hususani pale ambapo kunapojitokeza vyanzo hivyo kukauka.
Katika Swali lake la nyongeza, Mbunge huyo alitaka kufahamu mkakati wa Serikali wa kutumia maji ya mto rufiji ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji katika wilaya za mkoa wa Pwani.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA