TANZANIA NDIO CHIMBUKO LA MWANADAMU NA SI KWINGINE DUNIA


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii katikati Maj. Gen. Gaudence Milanzi akita utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Onesho la Historia ya Chimbuko la Mwanadam lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DSM. Wanao shuhudia kuliani Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdala na kushoto ni mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez , Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dsm Bw Achiles Bufure.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Mh Anna Abdalla akilitazama moja ya fufu la Binadamu wa kale wanaosadikiwa waliishi takribani miaka Milioni 3.6 iliyopita.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na wageni wengine wakipata maelezo ya historia ya chimbuko la Mwanadamu kutoka kwa Maratibu wa Onesho hilo Dr Agnes Gidna.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Maj. Gen. Gaudence Milanzi na mwakilishi wa Balozi wa Spain nchini Bw Bw Guilaume M. Juarez wakiangalia kwa umakini mkubwa masalia ya wanyama wakale walioishi trakribani miaka Milioni 4 iliyopita.


Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii nchini Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesisitiza kuwa Tanzania ndio nchi pekee Duniani yenye ukweli wa kisayansi unaothibitisha kuwa ndipo binadamu wa kwanza alipo patikana na kuanza kusambaa maeneo mengine Duniani na si kama baadhi ya nchi zinavyo jitangazia kuwa uridhi huu wa kihistoria ni wao.

Ameyasema haya kati ufunguzi wa Onesho kubwa la Kihistoria lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni lenye kuonesha ukweli huu wa kisayansi uliotokana na Tafiti mbali mbali zilizo fanywa na watafiti Duniani kama ule wa Laetoli mwaka 1978 na mtafiti Dkt. Mary D. Leakey zinazo onesha nyayo ziliachwa na zamadamu anayeiitwa Australopithecus afarensis na ni ushaidi usiopingika wa zamadamu kutembea wima kwa miguu miwili takribani miaka milioni 3.6 iliyopia.

Akizungumza katika ufunguzi wa Onesho hilo kwaniaba ya Balozi wa Spain nchini Msaidizi wa Balozi wa Spain nchini Bw Guilaume M. Juarez alisema kuwa binadamu wote tunapaswa kuheshimiana kama ndugu kwani tafiti nyingi Duniani zinadhihirisha ukweli usiopingika kuwa binadamu wote duniani wametoka Afrika na ni Tanzania hivyo watu wote ni watanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof Audax Mabula na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Makumbusho ya Taifa Bi Anna Abdala, wametoa wito kwa watanzania wote hususani waliopo jijini Dar es Salaam hasa wazazi na watoto kuitembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la kujifunza uwalisia wa ubinadamu wao badala ya kutumia muda mwingi kwenye sehemu zingine za starehee.

Onesho hilo la Chimbuko la Mwanadamu lililopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Mtaa wa Shaban Robart mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM sambamba na maonesho mengine litakuwa wazi kuazia saa tatu asubuhi na kufungwa saa 12 jioni kila siku za Juma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA