WAFANYAKAZI WA TBA WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA USAFI



WAKALA wa Majengo Tanzania imesema tayari imekusanya zaidi ya asilimia 40 ya madeni waliyokuwa wakiwadai watumishi wa Umma waliopanga katika nyumba za serikali.

Akizungumza na waaandishi wa habari leo wakati wafanyakazi wa TBA wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam zilizopo nyumba hizo , wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma, Elius Mwakalinga alisema, kabla ya kulipwa kwa fedha hizo  TBA ulikuwa ukidai zaidi ya bilioni sita ambapo baada ya kutolewa kwa notisi ya kulipa tayari wamekusanya bilioni 2.6.

Amesema, bado shughuli ya kuwatoa wapangaji wengine linaendelea katika mikoa mbalimbali na katika Mkoa wa Dodoma wamefanikiwa kuwaondoa  wapangaji katika nyumba 27 huku Mkoa wa Mwanza shughuli hiyo kukwama baada ya kuibuka fujo kati ya mpangaji na mfanyakazi  wa Kampuni ya udalali ya Yono ambao ndio wasimamizi wa shughuli hiyo.

“Kazi yetu sisi sio kuleta vita tunataka fedha irudi ili tuendelee na ujenzi wa nyumba nyingine, tumesikitishwa na kitendo cha mpangaji wetu Mwanza ambaye aliamua kuleta fujo na kumshambulia mfanyakazi  wa kampuni ya udalali wa Yono wakati akiondolewa tunaomba tu wawe wastaarabu wanapotakiwa kuondoka au wakubali kulipa,” alisema Mwakalinga.

Aidha amesema ili kuondoa tatizo la ucheleweshwaji wa ulipaji kodi katika nyumba hizo kuanzia mwezi Julai wapangaji binafsi wataanza kulipa kodi kwa miezi sita huku watumishi wa umma wakiendelea kulipa kwa miezi mitatu mitatu.

Pia amesema TBA inatarajia wa kupeleka  mapendekezo serikalini ili kuona namna ya kuwasaidia watumishi wa umma ambao hawakuwa na uwezo wa kununua nyumba za serikali na walikuwa ni wapangaji ili waweze kuendelea kuishi katika nyumba hizo hata baada ya kustaafu.
 Mkurugenzi mtendaji wa Wakala wa Majengo nchini(TBA), Elius Mwakalinga akishiriki shughul ya kufanya usafi pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma leo  jijini Dar es salaam.
 wafanyakazi wa TBA wakifanya usafi wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya utumishi wa Umma leo jijini Dar es salaam. 
Usafi ukiendelea leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA