WATANZANIA WAPATA FURSA YA KUSHIRIKI MAFUNZO KUHUSU TSUNAMI



Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.
………………………
Kutokana na kuwa na athari kubwa ambazo zimekuwa zikisababisha majanga makubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeandaa mafunzo ya siku tano ambayo yatashirikisha watu mbalimbali nchini ili kuwapa elimu kuhusiana na majanga. 

Akizungumzia Mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Zulmira Rodrigues alisema kupitia mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kupata elimu kuhusiana na Tsunami ikiwa ni pamoja na madhara ambayo yanasababishwa na hivyo ni matarajio yao watakuwa mawakala wazuri kwa kusambaza elimu hiyo kwa Watanzania wengine. 

“Watu wengi wamepoteza maisha tukumbuke Tsunami la Japan zaidi ya watu 20,000 walipoteza maisha kwahiyo tunataka mafunzo haya yasaidie kufahamu ni kwa kiasi gani Tsunami linakuwa na madhara hata kama limetokea mbali na hapa,” alisema Bi. Rodrigues. 

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho alisema ni vyema kwa watanzania kupata elimu hiyo kutokana na madhara ambayo yamekuwa yakitokea ikiwemo Tsunami la mwaka 2004 ambalo lilitokea eneo lililombali na bahari ya Hindi lakini lilisababisha athari nchini na kusababisha vifo vya waogeleaji watano. 

“Mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa wananchi wote na mwezi Septemba yatafanyika mengine na yatahusisha watu wengi lengo kila Mtanzania ajue nini cha kufanya siku athari zikitokea wajue nini wanafanya ni muhimu kwa kila mtu kujua athari za Tsunami hata likitokea mbali,” alisema Dk. Chamuriho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.