4x4

WATU 20 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO MAREKANI


Takribani watu 20 wameuawa, huku 42 wakijeruhiwa katika shambulio lililotokea kwenye klabu ya usiku ya Pulse iliyopo mjini Orlando nchini Marekani usiku wa kuamkia leo.Polisi wamethibitisha kuwa mshambuliaji katika tukio hilo alikuwa na bunduki mbili, na aliwashika watu mateka na kufyatuliana risasi na polisi kabla ya kuuawa.Maafisa katika Jimbo la Florida wanasema kuwa wanalichunguza shambulizi hilo linalochukuliwa kuwa la kigaidi.Zaidi ya watu 42 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali kwa matibabu.
Klbau ya usiku ya Pulse ambapo shambulizi hilo limetokea inatambulika kuwa ya wapenzi wa jinsia moja.Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka eneo la tukio;

Post a Comment