YANGA YAUMIA KWA MAZEMBE BAO 1-0


Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
YANGA SC imevuna matunda ya malumbano badala ya maandalizi kufuatia kufungwa bao 1-0 na TP Mazembe ya DRC katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Yanga, baada ya Juni 19 kufungwa pia 1-0 na wenyeji MO Bejaia 1-0 nchini Algeria.
Shujaa wa Mazembe leo alikuwa ni Mereveille Boppe aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki Chrtistian Luyindama dakika ya 74.
Katika mchezo huo ambao mashabiki waliingia bure, Mazembe walionyesha kiwango kikubwa zaidi ya Yanga kuashiria kwamba walistahili ushin di huo.
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa TP Mazembe, Christian Luyindama leo Uwanja wa Taifa
Kiungo wa Yanga, Obrey Chirwa akiruka juu kupiga mpira katika mchezo wa leo
Mshambuliaji wa TP Mazembe, Mtanzania Thomas Ulimwengu (kushoto) akigombea mpira na beki Kevin Yondan
Kiungo wa Yanga Juma Mahadhi akiugulia maumivu baada ya kukwatuliwa na beki wa Mazembe, Luyindama (kulia)
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akimtoka beki wa Mazembe Adama Traore (kulia)

Pamoja na ubora wa Mazembe, lakini leo Yanga ilicheza chini ya kiwango, wachezaji wake wakionekana kabisa kucheza kwa woga na kutojiamini.
Shambulizi la maana la Yanga lilikuja dakika ya 44 tu baada ya mshambuliaji Mzimbabwe kufanikiwa kumzidi mbio na maarifa beki Luyindama na kumpasia kiungo Deus Kaseke aliyepiga nje akiwa amebaki na kipa, Sylvain Gbohouo Guelassiognon.
Kipindi cha pili, Mazembe walifunguka zaidi na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Yanga hadi kupata bao lao pekee.
Kiungo Mzambia, Obrey Chirwa hakuwa na madhara leo, wakati kiungo chipukizi mzalendo Juma Mahadhi alijitahidi ingawa hakuweza kumaliza mechi baada ya kuumia na kumpisha Geoffrey Mwashiuya dakika ya 69.
Kuelekea mchezo huo, Yanga ilitumia muda mrefu kulumbana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya matangazo ya Televisheni hadi wakaamua kufuta viingilio siku mbili kabla ya mechi. 
Yanga itahitimisha mechi zake za mzunguko wa kwanza za Kundi A kwa kucheza na Medeama ya Ghana Agosti 7 Uwanja wa Taifa pia.
Vikosi kamili vya leo ni Yanga; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Mahadhi/Geoffrey Mwashiuya dk69, Obrey Chirwa/Matheo Simon dk71 na Donald Ngoma.
TP Mazembe; Sylvain Gbohoud Guelassiognon, Jean Kasusula, Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Rodger Asale, Adama Traore/Deogratius Kanda dk76, Merveille Bope, Nathan Sinkala, Koffi Christian/Jose Bodibake dk80, Christian Luyindama na Thomas Ulimwengu.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO ILALA

DC MKURANGA AZINDUA MRADI WA MASHAMBA MJI YA NAMAINGO MSOLWA

TGGA WAMUAGA BOSS WA GIRL GUIDES AFRIKA KWA HAFLA KABAMBE

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo (+video)

WAGGGS AFRIKA WAIPONGEZA TGGA KWA KUONGOZA AFRIKA KUSAJILI GIRL GUIDES WENGI