JAJI MKUU WA TANZANIA, ZIARANI MAHAKAMA KANDA YA MOSHI, AZINDUA RASMI MAHAKAMA ZA MWANZO BOMANG’OMBE NA SIHA.


 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akilakiwa na Mhe. Aishieli Sumari, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi alipowasili Mahakamani hapo kwa ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utendaji kazi katika Kanda hiyo.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika ofisi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi.
 Mhe. Jaji Mkuu akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama, Kanda alipowasili mapema Julai 14, 2016 kwa ziara ya kikazi.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe iliyopo Wilayani Siha Manispaa ya Moshi. 
 Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo, Bomang’ombe. Mahakama ya Tanzania ipo katika maboresho mbalimbali yote yakilenga kuboresha huduma ya utoaji haki, moja ya kipaumbele cha maboresho hayo ni pamoja na kuboresha mindombinu yake kama majengo ya Mahakama, lengo ni kuwa na majengo ya Mahakama za Mwanzo katika kila Kata, Mahakama za Wilaya katika kila wilaya, mikoa na hata Mahakama Kuu.
 Mhe. Jaji Mkuu akipanda mti wa kumbukumbu katika  eneo la Mahakama ya Mwanzo Bomang’ombe baada ya kuizindua rasmi Mahakama hiyo ambayo itakuwa kimbilio la haki kwa wakazi wa eneo hilo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Moshi mara baada ya uzinduzi rasmi ya Mahakama ya Mwanzo Boang’ombe wilayani Hai. (Picha na Mahakama ya Tanzania).
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI