JK - UTAFITI WA KINA WAHITAJIKA KATIKA KUKUMBANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI AFRIKA



Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifungua mkutano wa tatu wa Sera za Mabadiliko ya Tabia Nchi jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Climate Strategies. Mkutano huo ilijumuisha watafiti na watunga sera 80 kutoka nchi zaidi ya 10 nje na ndani ya Afrika chini ya kauli mbiu "Kutekeleza Makubaliano ya Paris - Suluhu Mpya za Utafiti kwa ajili ya Nchi zinazoendelea." Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Chuks Okereke, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba akizungumza katika mkutano wa tatu wa Sera za Mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea jijini Dar es Salaam. Waziri Makamba amesema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi 175 zilikubali na kutia saini Makubaliano ya Paris Aprili 22 mwaka katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York ili kuweza kupunguza na kudhibiti utoaji wa gesi ya kaboni duniani.
Mwenyekiti wa Mkutano wa Sera za Mabadiliko ya Tabia Nchi Bw. Chuks Okereke kutoka Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Mkutano huu ni wa tatu kufanyika duniani na wa kwanza kufanyika barani Afrika baada ya London, Uingereza 2014 na New Delhi, India 2015. 
Washiriki wa mkutano wakiendelea kusikiliza mada mbali mbali kutoka wataalam wa mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huu umewaleta watafiti, watunga sera, na wadau wa mazingita kutoka sekta ya umma, binfasi na taasisi zisizo za kiserikali kutoka nchi 10 ndani na nje ya Afrika kuweza kujadili suluhu mpya za utafiti kwenye mabadiliko ya tabia nchi kwa ajili ya nchi zinazoendelea.
Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa tatu wa Sera za Mabadiliko ya Tabia Nchi iliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Climate Strategies. Dkt. Kikwete alifungua mkutano huo wa siku mbili jijini Dar es Salaam iliyojumuisha watafiti na watunga sera 80 kutoka nchi zaidi ya 10 nje na ndani ya Afrika chini ya kauli mbiu "Kutekeleza Makubaliano ya Paris - Suluhu Mpya za Utafiti kwaw ajili ya Nchi zinazoendelea." Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba, Mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Chuks Okereke, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU