JKCI YAFANYA UPASUAJI WA MOYO, MTOTO APANDIKIZWA BETRI YA UMEME WA MOYO (PEACEMAKER)

1Kutoka kushoto ni Dk Michael Valentine kutoka Marekani, Dk Godwin Sharau wa JKCI-Muhimbili, Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley na Dk Anjelan Muhozya wakifuatilia afya ya mtoto, Happiness John Josephat baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo LEO katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
2Baadhi ya madaktari wakifuatilia maendeleo ya mtoto, Happiness John Josephat kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo LEO katika taasisi hiyo.
3Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley akimwangalia mtoto wake, Happiness John Josephat baada ya kufanyiwa upasuaji LEO.
4Baadhi ya madaktari na wataalamu wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya shughuli ya upasuaji kufanyika.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
………………………………………………………………………..
Na John Stephen
Dar es Salaam, Tanzania. Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat ambaye amepandikizwa  peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa moyo wake.
Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri.
Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu.
“Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza.
“Tatizo la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo. Upasuaji umefanywa kwa ushirikiano wa madaktari wa moyo na madaktari wa matibabu ya moyo nikiwamo mimi (Dk. Godwin Sharau), Dk Michael Valentine kutoka Marekani,  Dk  Kisenge na Dk Sulende Kubhoja, Dk wa usingizi, Dk Anjelan Muhozya na madaktari wengine ambao wamesaidia katika upasuaji huu,” amesema Dk Godwin Sharau.
Mama wa mtoto huyo, Elitruda Eligi Malley ambaye ni mkazi wa Sakina-Raskazon mkoani Arusha amewashukuru madaktari wa Taasisi hiyo kwa kufanya upasuaji huo na mtoto wake kutoka salama katika chumba cha upasuaji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI