KIKUNDI CHA SARAKASI CHA BUTTERFLY CHAREJEA KUTOKA INDIA

saWasanii wa Kikundi cha Butterfly Arts Group kilichokuwa kinafanya maonesho ya sarakasi nchini India, Kulia ni kiongozi wa kikundi hicho Selemani Pembe, Mwanaidi Abdallah, Abdallah Mkumba<hamidi Mbwana na Salem Mbugio.
——————————————————–
Na Mwandishi wetu
KIKUNDI cha sarakasi cha Butterfly Arts Group kimerejea nchini juzi kutoka India kufanya maonesho ya sanaa ya sarakasi.
Katibu wa kikundi cha Butterfly Arts Group, Selemani Pembe alisema jana Dar es Salaam kuwa katika ziara yao ya kikazi nchini India iliyodumu kwa mwaka mmoja ilikuwa na mafanikio makubwa ambapo wasanii wote sita wa kikundi hicho wamepata mafunzo ya kutosha  ya kufanya maonesho ya sarakasi.
Pembe ambaye pia ni mwalimu wa Sarakasi nchini aliyewahi kuongoza vikundi vya sanaa vya DDC Kibisa, Muungano Culture Troup, Makutano Dancing Troup, Ujamaa Ngoma Troup alisema katika kipindi chote cha kuonesha sanaa ya sarakasi wamegundua kuna utofauti mkubwa kati ya sanaa za maonesho za Tanzania na India.
Alisema wacheza sarakasi wa India wanatumia vifaa vya kufunga juu ya jukwaa na kubembea juu kwa juu tofauti na hapa nchini ambapo hakuna kumbi za kufunga vifaa maalum kwa ajili ya kuonesha sarakasi hizo.
Pembe alisema pamoja na kasoro hizo sarakasi ya Tanzania imekubalika sana nchini India hasa staili ya kujenga maumbo (Pyramid, kujenga minara mbalimbali na kucheza ngoma za asili.
Alisema maonesho mengine yanayowavutia wanamichezo nchini India ni mchezo wa Limbo ambao mwanasarakasi anapita katikati ya moto chini ya bomba maalum ambalo limewashwa moto mkubwa na mchezo mwingine ni ule wa kupanda bomba kwa staili mbalimbali mithili ya nyani.
Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja walikuwa wakifanya maonesho na Kampuni ya New Rambo Circus inachofanya maonesho katika miji mbalimbali nchini India na nchi jirani.
Alisema wakiwa huko walifanya maonesho katika miji ya Pune, Bangalore, Gujirat, Mumbay na miji ya mipakani na nchi ya Nepal.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA