LOWASSA, MBOWE NA NAPE WAONGOZA KUUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MAREHEMU SENGA

 Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akifuatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Annastazia Wambura, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe pamoja na waombolezaji wengine wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, marehemu Joseph Senga, Sinza Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda kwao wilayani Kwimba, Mwanza kwa mazishi kesho.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Waombolezaji wakiiingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda wilayani Kwimba kwa mazishi.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Joseph Senga
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura akitoa heshima za mwisho
  Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Joseph Senga
 Mjane wa marehemu Senga, Winfrida Senga akiuaga mwili wa mumewe
 Mtoto wa marehemu Joseph Senga, Esther akiuaga mwili wa marehemu babake
 Mtoto Kapama Senga akisaidiwa alipokuwa akiuaga mwili wa babake
 Mwakilishi wa Chama cha Wapiga Picha za Habari Tanzania, Seleman Mpochi akitoa salamu za rambirambi pamoja na kuwasilisha mchango uliochangwa na wapigapicha kusaidia shuguli za mazishi za aliyekuwa mpiga picha mwenzanoa, marehemu Joseph Senga.

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akijdiliana jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
 Lowassa akiwa na Nape Nauye pamoja na Freeman Mbowe
 Familia ya marehemu Senga
 Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika akitoa salamu za chama hicho
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
 Waombolezaji wakiwa katika shughuli hizo
 Freeman Mbowe ambaye ni mmiliki wa gazeti la Tanzania Daima, akielezea pengo lililoachwa na marehemu Senga katika gaezeti hilo pamoja na Chadema
 Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi za serikali wakati wa kuuga mwili wa marehemu Senga
 Nape akaipeana mkono na Lowassa baada ya kutoa salam za rambi rambi
 Nape akiteta jambo na Mbowe

 Mbunge wa Jimbo la Sumve, wilayani Kwimba, Richard Ndassa, ambaye amewahi fanya kazi na marehemu Senga gazeti la Mfanyakazi, akiuaga mwili wa marehemu Senga
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na baadaye kuhamia Chadema, Mgeja akiauaga mwili wa marehemu Senga
 Mhariri Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Senga
 Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa akitoa heshima za mwisho  wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Senga
 Mpiga Picha wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia amewahi kufanya kazi na marehemu Senga katika gazeti la Mfanyakazi, Deus Mhagale akiuaga mwili wa marehemu Senga
 Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda, ambaye pia amewahi fanya kai na marehemu Joseph Senga gazeti la Mfanyakazi akiuaga mwili wa marehemu
 Waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiuaga mwili wa marehemu Senga
 Wafanyakazi wa Gazerti la Tanzania Daima waliokuwa wanafanyakazi na marehemu Senga wakiwambele ya jeneza la mwili wa Senga
 Wapiga picha wakiuingiza kwenye gari mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao, marehemu Senga

Baadhi ya wadau waliokuwa miongoni mwa waombolezaji. Kutoka kushoto ni, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tganzania, Matina Nkuru,  Muhidin Sufiani,Rukia Mtingwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanania, Jackson Mmbando

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI