MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA YAMTIA HATIANI MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANAHABARI MWANGOSI


Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauwaji  kufikishwa
Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo
Mtuhumiwa wa  mauwaji  ya  Mwangosi  akipakiwa  kwenye  gari  za  FFU
Msafala  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiz askari  mwenzao anayekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia  leo
Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo
Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo 

wakili kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo
wakili kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za   binadamu ((THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo

Siku ambayo  mwanahabari  Daudi  Mwangosi  alipouwawa
Askari  hao   wakimtoa mahakamani  hapo  leo  mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi
                               Marehemu  Mwangosi  enzi  za uhai  wake 
………………………………………………………………………………………………………
Na  MatukiodaimaBlog Iringa
MAHAKAMA   kuu  kanda  ya  Iringa   imemtia hatiani   kwa   kosa la  kuua bila  kukusudia  askari  Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa  G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kuuua
 mwaahabari  Daudi  Mwangosi   mwaka 2012 katika  kijiji  cha Nyololo  wilaya ya  Mufindi.
Huku   wakili  upande  wa jamhuri  katika  kesi  hiyo  Adolph Mwaganda akiiomba  mahakama   hiyo  kutoa
hukumu  ya  kifungo  cha maisha  jela  kwa askari  huyo ambae hata   hivyo  alisema upande wa  jamhuri  hauna
taarifa  za  makosa yoyote  aliyopata  kuyafanya.
 
Hata   hivyo  mahakamani hiyo  imesema  adhabu kwa mtuhumiwa   huyo kutokana  na kupatikana na  kosa
hilo la  kuua bila  kukusudia itatolewa  Julai 27  majira ya saa 4 asubuhi  mwaka  huu.
 Jaji  Dkt  Paul Kiwelo ambaye  anayesikiliza kesi  hiyo alisema mahakakamani hapo leo    kuwa kati
ya  vielelezo  vitano vyote  vilivyoleta  kama  ushahidi mahakamani  hapo  kwa ajili ya  kesi   hiyo  namba 54 ya
mwaka 2013  ni  kielelezo   kimoja  pekee  cha  ungamo  kwa  mlinziwa amani  ambacho  ndicho hakukuwa na  shaka   na ungamo hilo ndilo  lililomtia hatiani  asikari
huyo.
Alivitaja   vielelezo vilivyopelekwa kama  ushahidi   kuwa ni Ramani   ya eneo la  tukio,ripoti  ya
tabibu ,ungamo  la mlinzi  wa amani ,silaha  aliyoitumia  na  rejista ya  silaha  .
 
Hata  hivyo  alisema kuwa  idadi  ya  mashahidi  katika   kesi sioinayowezesha  kumtia  hatiani
mtuhumiwa  ila  kinachomtia hatiani  ni aina ya  ushahidi wenye uhakika ambao unatolewa na  kuongeza  kuwa katika  kesi  hiyo upande wa  jamhuri  ulishindwa kuleta mashahidi  stahiki zaidi ya kuwa na mashahidi  ambao ukiacha mlinzi wa amani mashahidi wote  ushahidi   wao una masahaka na  haoonyeshi kama mtuhumiwa  huyo ndio  aliyehusika na mauwaji .
“ Niseme baada  ya   kusikiliza  ushahidi  wote …..mtuhumiwa
kaonekana na kosa la …

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA