MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA APOKEA SALAAM MAALUM KUTOKA SUDAN YA KUSINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik aliyeleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia)akizungumza na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na  ujumbe wake walioleta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri
wa Biashara na Viwanda wa Sudan ya Kusini Mhe. Stephen Dhieu Dau Ayik pamoja na ujumbe wake ambao walileta ujumbe maalum wa Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na kupokelewa na Makamu wa Rais ,Ikulu jijini Dar es Salaam.
……………………………………………………………………………………………………………..
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemtumia ujumbe maalum Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuru kwa jitihada za serikali ya

Tanzania za kusaidia kupatikana kwa amani katika nchi hiyo.
Ujumbe huo wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir umewasilishwa nchini  na Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchi hiyo Stephen Dhieu Dau Ayik kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ikulu jijini Dar es Salaam Tarehe 27-Jul-16.
Waziri huyo wa Serikali ya Sudan Kusini Stephen Ayik amesema hali ya usalama kwa sasa imeendelea kuimarika kufuatia kusitishwa kwa mapigano kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Salva Kiir na wanajeshi wa watiifu wa Aliyekuwa Makamu wa Rais Riek Machar
Akipokea ujumbe maalum wa Serikali ya Sudan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha amani
inapatikana katika Taifa hilo changa barani Afrika ambayo itawezesha wananchi wa taifa hilo kufanya kazi za maendeleo kwa amani na utulivu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pia amezitaka pande hizo MBILI zinazohasimiana kuzingatia na kuheshimu mkataba wa amani waliosaini jijini Arusha mwaka 2015 uliolenga kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na kurejesha amani katika Taifa hilo.
Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo ya amani ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo ili kukomesha  vita ambavyo vimekuwa vikigharimu mali na maisha ya mamia ya wananchi wa Sudan Kusini 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI