MBUNGE MWAMOTO NA RC IRINGA HATMAYE WAPOKEA MADAWATI YA MFUKO WA JIMBO LA KILOLO .......


Mbunge  wa  Kilolo  Bw  Venance  Mwamoto  akikabidhiwa madawati  leo  la  Bi Malidadi  kwa  niaba ya  mkurugenzi wa Kilolo ,madawati  hayo yametengenezwa kwa mfuko wa  jimbo la  Kilolo kwa kiasi cha Tsh  milioni 30 awali madawati hayo yalikataliwa  kutokana na  kutengenezwa  chini ya  kiwango  ila  sasa yametengenezwa kwa  kiwango
Dc  Kilolo Asia Abdalah na timu ya  wataalam  wakijiridhisha na ubora wa madawati hayo ambayo sasa  yapo  safi
Mbunge  Mwamoto  akifurahia ubora  wa madawati  ya  mfuko  wa  jimbo la  Kilolo
Na MatukiodaimaBlog 
MADAWATI 745 ambayo yalitengenezwa na mfuko  wa  jimbo la  Kilolo kwa gharama ya  Tsh  milioni 30 zilizotolewa na mbunge  wa jimbo  hilo Venance  Mwamoto  ambayo  yalikataliwa na mbunge   huyo na  mkuu wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza yamekamilika  kutengenezwa kwa ubora  .

Akizungumza  baada ya  kukabidhiwa madawati hayo leo mbunge  Mwamoto  alisema  kuwa amekubali  kupokea  madawati hayo  baada ya  kufurahishwa na  ubora  wake  na  hivyo  imani  yake  kuona  walimu  wanasimamia  utunzaji  wa madawati hayo  ili  kuondokana na kero  tena  ya madawati  katika  shule  zote  za  wilaya ya  Kilolo.

Mbunge  Mwamoto  alisema  kuwa  kufuatia  uhaba  wa madawati  uliyokuwa  ukiikumba wilaya  ya  Kilolo na kama  sehemu  ya  utekelezaji wa agizo la Rais Dr John Magufuli  alilazimika kuidhinisha  pesa  kiasi cha  Tsh milioni 30  kutoka mfuko  wa  jimbo la Kilolo  ili  kuweza  kusaidia utengenezaji wa madawati  300 japo Halmashauri  ya  Kilolo kupitia wadau  wake  wa ndani na makusanyo ya ndani   waliweza  kuongeza  kiasi  cha Tsh  milioni 19 na kufanya kuwepo kwa kiasi cha  pesa  cha  Tsh milioni 49 ambazo  zilifanikisha  kutengeneza madawati zaidi ya 1000 .

Alisema  kuwa pamoja na kazi  nzuri  iliyofanywa na Halmashauri  hiyo katika kushughulikia kero  ya madawati katika wilaya  hiyo ya  Kilolo ila mafundi  ambao  walipewa kazi  ya  kutengeneza madawati hayo   hawakuwa wazuri kutokana na  kushindwa  kuifanya kazi  hiyo kwa ubora  uliotakiwa hivyo kupelekea  kufanya kazi  hiyo kwa  kiwango  cha  chini zaidi.

"Nililazimika kukataa madawati  40 ambayo yalipelekwa shule ya Msingi Nyanzwa na Igunda  baada ya  kuyaona hayana  ubora  na wananchi  kulalamika  kuwa ni mabovu  ukilinganisha na madawati  ambayo yalitengenezwa kwa nguvu ya  wananchi katika  vijiji  hivyo ......hivyo sikuwa tayari kupokea  madawati hayo hali  iliyopelekea mkuu  wa  mkoa wa Iringa kufika  kuona  madawati hayo na kulazimika kuyakataa madawati  yote 745  kwa  kutaka  yatengenezwe kwa ubora"

Mwamoto  alisema  kuwa amefurahishwa na usimamizi mzuri  wa mkuu wa wilaya ya  Kilolo na  timu  yake  ya  mkurugenzi  wa wataalam  wengine  ambao  wameweza  kuifanya kazi hiyo ya  kusimamia  ubora  kwa muda  mfupi  wa wiki tatu kinyume na  muda  ule wa mwezi mmoja  uliotolewa na mkuu  wa mkoa wa Iringa .

Hata  hivyo Mwamoto  alisema kuwa  yawezekana  wapo  watendaji ambao walimchukia kwa  yeye  kukataa madawati  hayo ila ukweli  alifanya hivyo kusaidia watoto wa wana Kilolo kutoendelea  kukaa chini na kuwa iwapo madawati hayo yangepelekwa  shuleni  bado  wananchi  wangebeba  dhamana ya  kuendelea  kuchangishana kwa ajili ya kuchonga madawati.

Kwa  upande  wake mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  alisema  kuwa  baada ya  mkuu  wa  mkoa wa Iringa kumpa  agizo  la kusimamia zoezi  hilo ndani ya mwezi  mmoja alilazimika  kuifanya kazi  hiyo kwa haraka  zaidi  ndani ya  wiki tatu  ili  kuona  wanafunzi  wote  wanakaa kwenye madawati .

Alisema  kuwa timu ya   wakuu wa idaraka katika wilaya ya  Kilolo  wameonyesha  ushirikiano mkubwa katika  kutekeleza agizo  hilo na kuwa baadhi  yao  walikuwa wanalala kwenye  karakana  zilizopewa kazi ya  kutengeneza madawati hayo  mapema kabla ya muda  waliopewa  na  mkuu  wa mkoa wa Iringa .

Wakati  mkuu  wa mkoa wa Iringa Bi Masenza  pamoja na kumpongeza   mkuu wa  wilaya ya  Kilolo na  timu yake kwa  kutekeleza zoezi la usimamiaji wa ubora wa madawati hayo bado  alimpongeza mbunge  wa Kilolo Bw Mwamoto  kwa  kubaini suala  hilo   huku akiwataka  walimu katika  shule  zote  kuhakikisha  wanatunza madawati hayo ili  kuondokana na adha  ya  kuchangia madawati  mara kwa mara .

" Nimeridhishwa na ubora  wa madawati  hayo na  yale  machache  ambayo  yalipelekwa mashuleni  wanaendelea  kuyarekebisha ili  yaweze  kufanana na haya  ambayo kweli  yapo  katika  ubora mzuri "
TAZAMA VIDEO CHINI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU