MCHEZO WA UTANGULIZI KOMBE LA RAMADHANI MASAUNI NA JAZEERA CUP KATI YA MEVETERANI WA KIKWAJUNI NA TIMU YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR ULIOFANYIKA UWANJA WA MNAZI MMOJA TIMU YA BARAZA IMESHINDA BAO 1–0.


Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya TAYI Tanzania Ndh Abdalla Othman Miraji wakati akihudhuria fainali za Kombe la Masauni and Jazeera lililofanyika jana usiku katika viwanja vya Mnazi Mmoja kati ya Kilimani na Kisimamanjongoo, kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa utangulizi kati ya Maveterani wa Kikwajuni na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo huo timu ya Baraza imeshinda bao 1–0. 
Timu za Baraza na Maveterani zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika wakati wa fainali hiyo Timu ya Maveterani wa Kikwajuni wakiongozwa na Mhe. Mbunge wa Kikwajuni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng Hamad Yussuf Masauni kulia na Timu ya Baraza ikiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Nassor Salum Jazeera.
Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape akisalimiana na wachezaji  wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao na maveterani wa kikwajuni Zanzibar.Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape akisalimiana na wachezaji  wa timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wao na maveterani wa kikwajuni Zanzibar.
Mhe Waziri wa Michezo Mhe Nape akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Hamad Masauni wakiwa na bashasha wakati wakisalimiana. 
Waziri Nape akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni kabla ya mchezo wao wa kirafiki na Timu ya Baraza la Wawakilishi ukiwa ni mchezo wa utangulizi wa Fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera. mchezo uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja jana usiku.
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe Rashid Ali Juma akizungumza wakati wa mchezo huo wa ufunguzi wa Fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera Cup na kumkaribisha Waziri mwezake wa Michezo Mhe Nape Mnauye, akiwa kulia kwa waziri.
Waziri wa Michezo Tanzania Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kabla ya kuaza kwa mchezo wa kirafiki wa utangulizi wakati wa fainali ya Kombe la Ramadhani Masauni and Jazeera Cup zilizofanyika uwanja wa mnazi mmoja jana usiku
Wachezaji wa Timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni wakimsikiliza Waziri wa Michezo Mhe Nape Mnauye akitowa nasaha zake kwa Wanamichezo waliohudhuria fainali hiyo na kuupongeza Uongozi wa Kamati ya Mashindano hayo Jimbo la Kikwajuni Zanzibar.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS