Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa
yenye sifa nyingi nzuri na kuthibitisha hilo haitakushangaza kusikia
majina makubwa yanayovuma katika nyanja za medani za siasa, muziki na
soka n:k.
Baadhi ya watu
maarufu ambao wameiletea sifa nzuri mkoa wa Morogoro ni pamoja na
mwanamuziki maarufu Mbaraka Mushekhe, Juma Kilaza huku katika muziki wa
kizazi kipya huwezi kukosa kumtaja mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi
(Afande Sele) wakati upande wa soka wapo akina Kassim Manga Mlapakolo,
Hassan Mlapakolo, Hussein Ngulungu, Gibbson Sembuli, Jella Mtangwa,
Zamoyoni Mogella, Malota Soma na Charles Bonoface Mkwasa bila kusahau
Mohamed msomali kocha.
Achia mbali wanamuziki na wanasoka
kuivumisha Morogoro na kuileta sifa kedekede ndani na nje ya Tanzania
wamo wanasiasa walioitangaza vyema wakiwemo Isack Mwesongo,Guntram
Itatiro,Alhaji Juma Ngasongwa, na wengine wengi.
Katika makala
haya mwandishi wetu anaingalia sifa nyingine zinayoweza kupata mkoa wa
Morogoro na…