MRADI WA USAID WA UIMARISHAJI WA MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI WAZINDULIWA LEO

Mtaalam wa fedha wa mreadi wa PS3 ambaye ndie msimamizi wa uzinduzi huo Mkoani Kagera, Abdul Kitula akielezea maeneo mbalimbali ambayo mradi huo utahusika na kufanya kazi. 

Kitula alisema PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. 

Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Kagera wakifuatilia uzinduzi huo.
Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akijibu na kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki.

  Mtaalam wa masuala ya Rasilimali watu kutoka Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Remmy Moshi akiwasilisha mada.
 washiriki wakifuatilia mada katika mkutano huo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
 Maofisa wa mradi wa PS3 waliobobea katika masuala ya utawala bora wakiwa katika mkutano huo.
  Mtaalam wa Mawasiliano na Takwimu wa Mradi wa PS3, Desideri Wengaa akitoa mada juu ya mawasiliano na utoaji takwimu sahihi.
 Maofisa kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo.
 Mshiriki akifuatilia mada kwa umakini.
 Waandishi wa habari wakifuatilia matukio.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango.

Mratibu wa Mafunzo ya muda Mfupi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambao ni moja wa wadau wa utekelezaji wa mradi huo wa PS3, Benjamin Magori akifafanua baadhi ya mambo.

 
 Picha ya pamoja ya makundi mbalimbali.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu (katikati) akiwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa huo.
 Picha ya pamoja katika ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Maofisa wa PS3.
*********
UZINDUZI wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), umefanyika mjini Bukoba mkoani Kagera siku ya Jumanne na Jumatano, leo Julai 12-13, 2016. 

Mradi huo ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening (PS3) ni wa miaka mitano, na utafanya kazi na Serikali Kuu pamoja na Halmashauri 93 katika mikoa 13 ya Tanzania bara.

PS3 inalenga kuunda ushirikiano na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti tendaji. 

Ushirkiano huu wa PS3 katika ngazi ya Serikali kuu na Halmashauri, una nia ya kukuza utoaji, ubora, na matumizi ya huduma za umma, hususan kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.

Katika uzinduzi huo, mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja.Jenerali (Mstaafu), Salum Kijuu na unawashirikisha watemdaji  takribani 200. 

Washiriki wa uzinduzi huo walikuwa ni: Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Wakuu wa Wilaya za Kagera, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, na Wajumbe wa Timu ya Mejenimenti kutoka kwenye Halmashauri. 

Mkoa wa Kagera una Halmashauri nane, ambazo ni: Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Halmashauri ya Mji wa Karagwe, Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.

PS3 ni mradi wa miaka mitano ambao umeandaliwa na USAID kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania, na unafadhiliwa na USAID. 

Unatekelezwa na mashirika saba yakiwepo ya kitaifa na kimataifa, ambayo ni: Abt Associates Inc., kama mtekelezaji mkuu, na watekelezaji wasaidizi ambao ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzi ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International, na Urban Institute. 

Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga.

PS3 itaimarisha mifumo katika ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. 

Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Mafanikio yanayotarajiwa ni pamoja na:

Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Raia: Uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta.

Rasilimali Watu: Kuongezeka kwa usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini.

Fedha: Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa.

Mifumo ya Mawasiliano: Kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini, pamoja na matumizi ya takwimu kwa wadau.

 Utafiti Tendaji: Tafiti Tendaji muhimu zitakazosaidia mradi kujua changamoto na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizo. 

Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa.Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU