NASHUKURU MUNGU KWA KUUTUA MZIGO SALAMA HUKU NIKIICHA NCHI IKIWA SALAMA TULII KABISA-JK

jk1Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete
akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya
kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika
wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
jk2Wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi wakimsikiliza Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete katika hafla ya
kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM,iliyofanyika wilaya
ya Bagamoyo.PICHA NA MICHUZIBLOG
……………………………………………………………………………………………………………
Na David John Pwani
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete
amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama huku akiicha nchi
ikiwa salama tulii kabisa.
Amesema kuwa safari yake ya urais  ilianzia Bagamoyo akitokea wilayani hapo ambapo baada ya hapo
alikwenda Kibaha kutangaza nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia
flaha kurudi tena Bagamoyo akiwa salama.
Amesema wakati  akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa na mtoto wake Ridhiwani
Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika na Ridhiwani anachapa kwenye
Komputa.
Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka  mingi, ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani.
Alisema.anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na kwamba amemaliza salama na
ameacha nchi ikiwa salama na imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi.  Akikumbuka mchakato wa mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo  mengi lakini mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .
“Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na  wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi”amesema Dkt.Kikwete  .Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo kulikuwa hakuna mtu
ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake hali ambayo iliwashangaza
hata nchi jirani.
Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi  amefanya kazi kubwa ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa  yote,wilaya zote bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na  Changamoto ya kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka  maendeleo Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa  hawana haki.
Aidha Dkt.Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha  fedha za ujenzi wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita, Sengerema,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na
hadi kufikia wabunge kulumbana.
Amesema hata hivyo anashukuru  kwamba amemaliza salama na Kwa Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana  ari kubwa ya kuwaletea maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga
mkono. Wanachana
Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama hicho Dkt.Jakaya Kikwete katika sherehe  zilizofanyika wilayani Bagamoyo. Wanachama hao ambao walitoka katika  wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho  mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga walimuaga na kumkaribisha
Kwa nyimbo mbalimbali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI