NEMC YAPEWA MWEZI MMOJA KUKAMILISHA RIPOTI YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KATIKA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA MTWARA


2Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina akipata Maelezo kuhusu uchataji wa taka unaofanywa na kiwanda cha SBS kutoka kwa  Bw. Joseph meneja uendeshaji wa kiwanda hicho.
3Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kulia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw.  Khatibu Kazungu  kushoto ni  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda wakigagua DAMPO jipya la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira.
1DAMPO la kisasa la Mjini Mtwara ambalo ni rafiki kwa mazingira lililojengwa kwa hisani ya benki ya Dunia kwa thamani ya shilingi bilioni 8.8, mara DAMPO hilo litakapoanza kutumika litakuwa na uwezo wa kutengeza nishati mbadala.
(Picha na Evelyn Mkokoi)
………………………………………………………………………………………………
Baraza la taifa na Hifadhi ya Mzingira NEMC limepewa mwezi mmoja na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kupima Vumbi, Moshi na Maji yanayotoka katika kiwanda cha kuchakata taka cha SBS kilichopo katika maeneo ya Mangamba Mjini Mtwara ili kujirisha kama vina madhara kwa mazingira na viumbe hai.
Naibu Waziri Mpina akiwa katika muendelezo wa Ziara yake ya kukagua mazingira na kuangalia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa wenye viwanda nchini amelitaka baraza hilo kufanya kazi zake kwa umakini na kutokukubali majibu ya vipimo toka kwa mwenyekezaji bila NEMC pia kufanya vipimo na kupata majibu sahihi kutokana na sababu kuwa wananchi wamekuwa wakilalamika mara kwa mara juu ya uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wenye viwanda jinsi unavyo hatarisha maisha yao na mazingira kwa ujumla.
Katika Ziara Hiyo ya Mjini Mtwara, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea DAMPO la kisasa la mjini hapo lilijengwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia lenye thamani ya shilingi Bilioni 8.8 na kuwapongeza wana Mtwara kwa kupata Dampo la kisasa ambalo ni Rafiki wa Mazingira, na kuwashauri waratibu wa mradi huo na uongozi wa mkoa wa Mtwara kuanza kutumia DAMPO hilo ambapo taka zitakazowekwa katika DAMPO hilo la kisasa, pia zinaweza kutumika kutengeneza nishati mbadala.
Awali, akitoa taarifa ya Mazingira ya Mkoa wa Mtwara, katibu Tawala wa Mkoa huo Bwana Afred Luanda, alisema kuwa Mkoa unakabiliana na changamoto mbali mbali za kimazingira ikiwa ni pamoja na uvuvi haramu wa kutumia mabomu, ukataji miti ovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa, vifaa vya uondoshaji taka pamoja na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziara Ya naibu Waziri Mpina Mkoani Mtwara leo ilihusisha pia kutembelea bandari ya mtwara ili kujionea utekelezaji wa sheria ya mazingira katika uingizwaji wa viwatilifu na kemikali hatarishi kwa mazingira zinazoingizwa  kupitia bandari hiyo.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS