PROFESA NTALIKWA AELEZEA MIKAKATI YA UZALISHAJI UMEME

nta1Mwenyekiti kutoka  Taasisi ya  Daima Associates Ltd, Profesa Samuel Wangwe (kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa Nishati kwa Ukuaji wa Uchumi  ulioshirikisha wadau wa nishati kwa ajili ya kujadili  utafiti wa sekta ya nishati unaotarajiwa kufanyika nchini miaka mitano ijayo.
nta2Mwenyekiti kutoka  Taasisi ya  Daima Associates Ltd, Profesa Samuel Wangwe akielezea Mpango wa Nishati kwa Ukuaji wa Uchumi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) kwenye mkutano uliokutanisha wadau wa nishati  jijini Dar es Salaam.
nta3Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kulia) na washiriki wengine wakifuatilia mada iliyokuwa inawakilishwa na Profesa Catherine Wolfram kutoka Chuo Kikuu cha California, Berkeley (hayupo pichani) katika mkutano huo.
nta4Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa akizungumza mbele ya washiriki kwenye  ufunguzi wa mkutano wa Nishati kwa Ukuaji wa Uchumi  ulioshirikisha wadau wa nishati kwa ajili ya kujadili  utafiti wa sekta ya nishati unaotarajiwa kufanyika nchini miaka mitano ijayo.
nta5Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akifungua mkutano wa Nishati kwa Ukuaji wa Uchumi  ulioshirikisha wadau wa nishati kwa ajili ya kujadili  utafiti wa sekta ya nishati unaotarajiwa kufanyika nchini miaka mitano ijayo.
nta6Profesa Catherine Wolfram kutoka Chuo Kikuu cha California, Berkeley akielezea changamoto za sekta ya nishati Afrika Mashariki  katika mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………..
Na Greyson Mwase,
Imeelezwa kuwa nishati ya umeme  inatarajia kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji  wa uchumi wa nchi kupitia  kuongezeka kwa uwekezaji kwenye  viwanda.
Hayo  yalielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa  wakati akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya  Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo kwenye mkutano  wa Nishati kwa Ukuaji wa Uchumi  uliokutanisha wadau mbalimbali wa nishati kwa ajili ya kujadili  utafiti kuhusu  sekta ya nishati  unaotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia sasa nchini Tanzania.
Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam  uliandaliwa na  Kituo cha Usimamizi wa Sera cha Oxford kwa kushirikiana na  Shirika la Misaada la Uingereza, na  wawekezaji binafsi katika sekta ya nishati   nchini.
Profesa Ntalikwa alisema  Serikali  imeweka mikakati  katika  kuhakikisha kuwa   umeme wa uhakika unapatikana kwa gharama nafuu na hivyo kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Akielezea  historia ya uzalishaji wa umeme nchini, Profesa  Ntalikwa alisema kuwa mwaka 2005 ni asilimia  10 tu  ya wananchi walikuwa wanapata umeme  hali iliyopelekea Serikali kuweka mikakati mbalimbali  ikiwa ni pamoja na  uanzishwaji wa Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) wenye  jukumu la kusimamia miradi  yote ya usambazaji wa umeme  vijijini.
Aliendelea kusema hadi sasa  ni asilimia 40 ya wananchi wanapata umeme na kusisitiza kuwa bado  serikali  imeendelea kuweka mikakati ya matumizi ya vyanzo  vya nishati  ili kuzalisha umeme wa uhakika.
Alitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na  uanzishwaji wa miradi   ya uzalishaji umeme kwa njia ya  gesi ikiwa ni pamoja na  upanuzi wa kituo cha Kinyerezi I (Megawati 185), Kinyerezi II (Megawati 240), Kinyerezi III ( Megawati 300) na Kinyerezi IV (Megawati 330) ambacho kiko  katika hatua ya mwisho ya maandalizi yake.
Aliendelea kutaja miradi mingine kuwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia gesi cha  Somanga Fungu (Megawati 320) ambapo wawekezaji wanahitajika na kituo cha Mtwara (Megawati 600) ambapo upembuzi  yakinifu unaendelea bado
Alitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na mradi wa umeme wa upepo wa Singida (Megawati 100), Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Makaa ya Mawe wa Kiwira ( Megawati 200) unaomilikiwa na  Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) ambapo mbia anakaribishwa kuendeleza mradi huo.
“Kuna mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma (Megawati 400) na Ngaka (Megawati 200) chini ya  Shirika la Maendeleo la  Taifa (NDC) ambapo wawekezaji wanakaribishwa,” alisema Profesa Ntalikwa
Alisema  Tanzania ina vyanzo  vingi  vya nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na gesi, maji, upepo, jotoardhi, makaa ya mawe na kuwakaribisha  wawekezaji kwa ajili ya kuchangamkia  fursa zilizopo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU