Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya | Ulinzi na Usalama, Rais John | Magufuli akiweka mkuki kwenye Mnara | wa Mashujaa wakati wa Maadhimisho | ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa | mjini Dodoma |
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli akitoa heshima baada ya kweka mkuki na ngao kwenye Mnara wa Mashujaa wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Tanzania Legion askari wa zamani waliopigana Vita vya Pili vya Dunia wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma
Wananchi wakishangilia wakati Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli akisalimiana na kuwaeleza kuwa atahakikisha ndani ya miaka minne na miezi minne ya uongozi wake atahakikisha serikali yake itahamia Makao Makuu Dodoma.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akihutubia na kusisitiza wananchi kudumisha amani wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma
Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika maadhimisho hayo
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Viongozi wa vyombo vya ulinzi na Uslama wakielekea kumpokea Rais John Magufuli,Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Othman Rashid, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mwenyekiti wa Parole Tanzaia, ambaye pia ni Mwenyekiti cha chama cha Upinzani cha TLP, Augustino Mrema (kulia) akiwa miongoni mwa viongozi waalikwa katika maadhimisho hayo
Askari wa JWTZ wakipiga buruji wakati wa maadhimisho hayo
Wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo
Rais John Magufuli akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho hayo
Comments