SERIKALI YAPONGEZWA KWA KUWAJALI WATU WENYE MAHITAJI MAALUM


1Wakonta Kapunda : Msichana mwenye umri wa miaka (22) akitumia ulimi kuandika meseji kwenye simu yake ya Mkononi  wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Dada yake Bi. Judith Assenga.Binti huyo ameanza kutumia kiungo hicho katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutokana na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa wakati wa Mahafali ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe Mkoani Tanga.
2Msichana mwenye umri wa miaka (22) Bi. Wakonta Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Binti huyo anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
3Judith Assenga(kushoto) dada yake na Wakonta Kapunda akimuelekeza jambo mdogo wake  wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wakonta anatumia ulimi na simu aina yaSmart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
4Mratibu wa Masuala ya Habari katika Kampeni ya kumsaidia Wakonta Bw. Joseph Kithama akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Binti huyo anayehitaji msaada ili apatae matibabu na kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.
5Kutoka kulia ni Wakonta Kapunda, Judith Assenga(dada yake na Wakonta), Mwajuma Selkemani na Chritina Rubangula(waliokuwa wanafunzi wenzake na Wakonta) wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani Tanga.
6Baba mzazi wa Wakonta (hayupo pichani) Bw.  Brazilio Kapunda akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa Radio ya Kimataifa ya Ufaransa (Rfi) wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.Mwenye brauzi nyekundu ni Mama wa binti huyo Bibi. Rahel Lymo,Wakonta anatumia ulimi na simu aina ya Smart Phone katika kuandika baada ya kupooza sehemu ya mwili wake kutoka na ajali mbaya aliyoipata mwaka 2012 akiwa na wenzake tisa Korogwe Mkoani
7Waandishi wa habari wakiwa wameshika karatasi lenye namba ambazo wadau wanaweza kutumia kumchangia Wakonta Kapunda (aliyekaa kwenye kiti cha matairi) ili apatae matibabu na hatimaye kutimiza ndoto zake za kwasaidia wengine wenye matatizo kama yake leo jijini Dar es Salaam.Binti huyo amekusudia kutumia kalama ya uandishi wa Filamu na kuanzisha Taasisi itakayo kuwa msaada kwa watu wenye matatizo ya kupooza.
8Wakonta Kapunda akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake,Dada yake, marafaiki zake aliosoma nao shule ya Sekondari Korogwe na mshiriki mwenzake katika Shindano la uandishi wa Miswada lililofanyika mjini Zanzibar leo Jijini Dar es Salaam.
Picha Zote na: Frank Shija, MAELEZO.
……………………………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
Msichana anayetumia Ulimi katika kuandika miswada ya Filamu amewashukuru wadau mbambali kwa misaada yao iliyomfanikisha kuweza kushiriki katika mashindano ya uandishi wa miswada ya Filamu yaliyofanyika mjini Zanzibar.
Shukuruani hizo amezitoa leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anaongea na waandishi wa habari kuhusu malengo yake ya kuanzisha Taasisi itakayosaidia watu wenye matatizo kama yake.
Wakonta amesema kuwa kwa namna ya kipekee kabisa anaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia kwa Bodi ya Filamu kumgharamia nauli iliyomsaidia kutoka kijijini kwa Kipili wilayani Nkasi mkaani Rukwa hadi kuanikisha ushiriki wake katika mashindano hayo.
“Ninaishukuru sana kwa kipekeke Serikali ya awamu ya Tano, kwani kupitia kwa KatIBU Mtendaji wa Bodi ya Filamu nimeweza kusaidiwa fedha iliyoniwezesha kushiriki katika mashindano ya Uandishi wa Miswada ya Filamu nashukuru sana”. Alisema Wakonta.
Aliongeza kuwa pamoja na Serikali kumpa msaada huo wapo baadhi ya wadau ambao nao wametoa michango yao katika kufanikisha Kampeni yake ambapo amewataja wadau hao kuwa ni Clouds Media waliomsaidia kuhabarisha umma, Joyce Kiria aliye safiri hadi kijijini kwao Kipili ili kumsaidia kupitia kipindi chake cha Wanawake Live.
Wengine ni pamoja na magazeti ya Mwananchi na Uwazi kupitia waliokuwa msaada kupitia  habari zao, Fastjet waliomsaidia huduma ya usafiri kutoka Mbeya na Hoteli ya Serena waliomsaidia upande wa malazi wakati alipofika Dar es Salaam akitoea kijini kwao Kipili, Mkoani Rukwa.
Ametoa rai kwa wadau wenye nafasi zao kujitokeza na kushirikina naye katika kukuza kipaji chake ili aweze kukitumia katika kuleta tija kwa Taifa kwani kupitia Filamu unaweza kutangaza Utalii wanchi na ata biashara.
Wakonta alikuwa miongoni mwa washiriki 15 kutoka Afrika Mashariki katika Shindano la  Uandishi wa Miswada ya Filamu la Maisha Scree Writer’s Laboratory Course lililofanyika mjini Zanzibar na huku yeye akiwa mshiriki pekee anayetumia Ulimi katika kuandika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.