TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) YAZINDUA KAMPENI YA NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI KWA WASAMBAZAJI WAKE NCHINI.

TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) YAZINDUA KAMPENI YA NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI KWA WASAMBAZAJI WAKE NCHINI.

 Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George kavishe akiongea na baadhi ya mawakala wakati wa uzindinduzi wa kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake .Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa Protea jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa mawakala wa kampuni ya Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL), Bi.Grace Ulomi akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi
 Meneja Masoko na udhamini wa TBL Group, George Kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzindinduzi wa kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake .Wengine pichani ni  Maofisa wa kampuni hiyo.
Baadhi ya mawakala waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo. --- Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, leo imezindua rasmi kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake itakayodumu kwa muda wa wiki 12. Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Protea Oystebay - Dar es salaam, Mwakilishi wa Kampuni ya TDL, Meneja Masoko na Udhamini Bwana George Kavishe alisema; “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck). Tunaamini kwa magari haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo yao ya mauzo” Pia, kupitia shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea kusema. Naye Meneja Mkuu wa TDL; Devis Deogratius alisema “Katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa zetu wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi baada ya miezi 10. Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.