VIJANA WAASWA KUACHA KUSUBIRI FURSA MAJUMBANI.

IMG_0319
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Je nista Mhagama
……………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Vijana wameaswa kuacha kukaa majumbani na kusubiri fursa za maendeleo ziwafate walipo na badala yake watumie muda mwingi kujishughulisha kwa kufuata fursa zilipo ili kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha taarifa ya utafiti wa Sauti za Vijana Tanzania Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana ,Ajira na walemavu Mhe. Je nista Mhagama amesema kuwa vijana wasikae majumbani na vijiweni kutegemea Serikali iwapelekee fursa hizo.
“Vijana tusikae majumbani na kushinda vijiweni tukitegemea kwamba tutawaletea fursa huko mlipo , mnatakiwa mtoke na mtumie muda wenu kufikiri jinsi ya kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutumia fursa zitolewazo” alisema Mhe. Mhagama.
Aidha Mhe. Jenista alisema kuwa  Serikali imeanza kutenga Shilingi Bilioni 15 kila bajeti kwa ajili ya kukuza ujuzi na kujikwamua kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa vijana na taifa kwa ujumla.
Mbali na hayo Mhe. Mhagama aliunga mkono kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwamba ni marufuku kwa kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani kinaharibu nguvu kazi ya vijana wa leo.
“Nasisitiza tena marufuku kwa  kumbi za starehe na mahali popote kuuza kilevi aina ya shisha kwani inaharibu uwezo wa kufikiri kwa vijana na kushindwa kufanya kazi matokeo yake uchumi wa nchi unazorota ,kwa yeyote atayekiuka maagizo haya hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Aidha Mhe. Jenista aliwataka vijana kutumia vizuri fursa iliyotolewa na Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa Shilingi Milioni 50 kwa kila kijiji ili kuleta chachu ya maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.