Vijana wajisajili Airtel Rising Stars 2016


Hamza Hemed kutoka Twalipo Youth Academy akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally.
Farid Ally kutoka Mbangala Youth Academy FC akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally.
Hamisi Nassoro kutoka Carpet FC akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa Temeke Kassim Ally
 XXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM

Usajili wa wachezaji kwa ajili ya mashindano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars 2016 umeanza leo katika mikoa inayoshirikia michuano hiyo mwaka huu ambapo mashindano katika ngazi ya mkoa yamepangwa kuanza wiki ijayo Julai 30.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchi TFF, michuano hiyo ngazo ya mkoa inatarajiwa kumalizka Agosti 28 na kufuatiwa na mashindano ya taifa yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi 11.

Akiongea wakati wa usajili katika mkoa wa kisoka wa Temeke, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira Temeke Kassim Mustafa alisema mkoa wake wamejiandaa vema kwa ajili ya kutetea ubingwa walioshinda mwaka jana. “Leo tumeanza usajili wa wachezaji kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Airtel kwa mradi wake huu wa kusaka na kukuza vipaji vya soka kwa vijana wetu. Temeke tunao vipaji vyingi na ndio sababu mkoa wetu uliweza kushinda taji la ARS 2015,” alisema Mustafa.

Naye kocha mkuu wa Twalipo Youth Academy Neville Kanza alisema anafurahi ujio wa Airtel Rising Stars 2016 huku akisema vipaji vipo vingi na kutamba kuendelea kutoa vijana wengi kwenye kombaini timu ya mkoa. Mwaka jana Twalipo academy ilitoa wachezaji watano ambao waliunga timu ya taifa ya Airtel Rising Stars Dream Team.

Kwa wake Ofisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde alisema wanayo furaha kuona vijana wameweza kufanikisha ndoto zao kwa kupitia michuano ya Airtel Rising Stars. “Ni furaha kuona timu zetu za taifa zikiwa na wachezaji ambao wametoka na program hii ya Airtel Rising Stars,” alisema na kuongeza kuwa hii ni fursa nyingine kwa vijana kujitokeza kwenye usajili ambao utawawezesha kushiriki michuano hii na kuonyesha vipaji vyao.

Alisema Airtel Rising Stars mwaka inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili kujiendeleza kiuchumi. “Airtel Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa inawawezesha vijana kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira. Mpira ni chano cha kipato cha kuaminika”, alisema.

Mikoa inayoshirikia mwaka huu ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mwanza, Mbeya na Morogoro (wavulana) na Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Lindi na Zanzibar zikishirikisha wasichana.

0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

ANGALIA PICHA NDEGE KUBWA YA ABIRIA DUNIANI ILIYOANZA SAFARI NDEFU ZAIDI!

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA CHAKE CHAKE,MKOA WA KUSINI PEMBA LEO.

NCHI YA URUSI NDIYO NCHI INAYOONGOZA KWA KUWA NA UBORA WA ELIMU NA VYUO DUNIANI.